GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

Jua kwanini shetani anapenda kuwatumia viongoz wako kukuvuluga?

Tulikua na kichwa kinachosema NAMNA YA KUPAMBANA NA NGUVU ZA GIZA na tuliishia kwenye kipengele cha njia anazozitumia shetan kupandikiza ufalme wake Duniani.. Tuliangalia kwa habari ya
✍makanisa
✍fedha
✍muziki
Leo tutaangalia kwa habari ya
✍Viongozi
shetani wakati mwingine anapotaka kupitisha jambo la kishetan huwatumia watu wenye madaraka juu yetu.. Watu ambao anajua wana madaraka makubwa sana kwetu.. Na kupitia kauli zao hata kama hazimpendezi Mungu kama hujasimama Na Mungu unaweza kuzikubali.. Angalia kipindi Musa anazaliwa . farao alitoa tamko la watoto wote wa kiebrania  kuuliwa..na musa alikua ni muebrania.. Shetan alishajua kile Musa amekuja kukifanya na ndiyo maana aliona njia kubwa ya kuthitisha ukombozi wa waebrania ni kutumia kinywa cha mfalme wa misri na akatoa tamko ambalo lilikua linamfunga Musa moja kwa moja..
Angalia Yesu alipozaliwa..herode anatoa tamko la watoto wa kiume kuuuliwa .. Shetan alijua kuwa Yesu amezaliwa kuja kufanya nini na anaamua kumtumia herode kama kiongozi mkubwa kutoa tamko la kuuwawa lakini malaika anamtokea yusuph katika ndoto na kuwaambia watoke katika nchi sababu Herode  anataka  kumuua mtoto..
Kauli ya viongoz inanguvu sana .. Na kama hujasimama vizuri na Mungu unaweza kuogopa na kuwafata hao viongozi kile wanachosema kwa kuogopa madaraka yao.. Lakini jifunze kwa kina Daniel waliitetea iman. Hawakukubali kumsujudia yule sanamu mpaka wakatumbukizwa kwenye tanuru la moto bado waliendelea kutetea kile wanachokiamin..
Mathayo 10:28

" Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum"

Ni aibu sana mkristo kutii kile unachoona kina pingana na wokovu ili tu kuwapendeza wanadamu au viongozi wako.. Yesu anasema tusiogope wale wanaoweza kuangamiza mwili tu.. Ila tuogope Mungu anaeweza kuangamiza mwili na Roho pia..
Usikubali kusujudia miungu mingine kwa kuogopa viongozi wako..
✍sio kila kiongozi anaweza kusema lililo kusudi la Mungu wengine husema yalio makusudi yao..

📌Misaada mbalimbali
Sio kila masaada unaotolewa unakua umelenga kutusaidia.. Mwingine ni kwaajili ya kupitisha maagano ambayo yatatufanya kwenda kinyume na Mungu.. Kumbuka kuwa msaada ni kama sadaka mtu anaitoa.. Je unajua amenenea nini hiyo sadaka?!  Sio kila msaada lazima upokee.. Hata ukiupokea basi kumbuka kuombea.. Umepewa neti za bure toka Usa basi unapozipokea kabla hujatumia zitakase kwa damu ya Yesu sababu hujui hiyo sadaka imenenewa nini.. Sikia kunasadaka nyingine huambatana na  mapepo.. Au manuizo ya kipepo..
Wakati mwingine unaweza jiuliza kwanini kuna umwagaji wa damu mwingi au ajali nyingi.. Wakati mwingine ni kwasababu kuna sadaka imetolewa au maagano yamefanyika ambayo yanampa adui uhalali wa kumilili..

✍Jifunze kuombea sadaka au zawadi yoyote mtu anayokupa. Sababu nyuma ya hiyo sadaka au zawadi lipo lengo jema au baya.. Pia sio kila wakati ni lazima kukubali kupokea msaada,  Roho mtakatifu akikuzuia acha usipokee hata kama unauhitaji na hicho kinachotolewa

✍Jifunze kuombea viongozi wako wa nchi na Bunge pia  ili maamuzi wanayoyafanya yaendane na kusudi la Mungu sio la kishetan..
Pia kumbuka sio kila mkataba unaso sainiwa ni sahihi.. Hivyo omba hekima kwa MUNGU juu ya viongozi ili Mungu aachilie hekima kwao..

Angalia tu kwa suala la ndoa za jinsia moja .. Shetani ametumia viongozi wa nchi kulipitisha pamoja na ushoga.. Lakini ashukuriwe Mungu sababu Tanzania viongozi wetu walilikata jambo hilo..
Pia unaweza kukumbuka kwa habari ya mahakama ya kazi .. Lakini nikukimbushe MTU wa Mungu.. Usisubiri mambo yaharibike ndo uanze kuomba au uchaguzi ufike ndo uanze kuomba .. Nooo muda ni huu wa kuomba anze leo wakati aman ipo..
Muombe rahis hata kama hukupenda awe yeye sababu bado maamuzi yake yana nguvu kwako pia..

📌Migogoro ya kidini
Hi ni mbinu nyingine ambayo adui anaitumia kujenga ufame wake dunia.. Akitaka tu watu waache kumtafuta Mungu anaingiza migogoro ya dhehebu hili na lile au kanisa hili na lile ili tu tutumie muda mwingi katika kukosoana na kuonesha nani ni bora kuliko mwingine badala ya kutumia huo muda kujifunza Neno la Mungu kwa undani.. Huu ni mpango wa adui ulio halisi kabisa..
Ngoja nikwambie mpendwa dini au dhehebu ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu lakini wokovu ni  mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu.. Sasa unapotumia muda mwingine kutafakari kwa dini au dhehebu lipi ni sahihi utakuwa unapoteza muda sababu hakuna dhehebu lililokamilifu lisilo na  mapungufu  na madhehebu yapo na yatazidi kutokea mengine na hata ukiondoka dunian utaayacha lakini Yesu yeye ni yule yule Jana leo na milele.. Tumtafakari huyo.. Huku msingi wetu ni Biblia takatifu Roho mtakatifu ndiye mwalimu mzuri wa Neno..
✍usipoteze muda kufikiria dhehebu lipi ni sahihi ili uende huko ila anza kushugulika nawewe kwanza kisha muombe Mungu wapi anapenda ukasali .. Kisha nenda huko.. Unaweza kuhama hata makanisa mia lakini kama tatizo ni wewe kamwe Usitegemee kupata uvumbuzi wa tatizo lako na kuna hatari Yesu akakukuta upo kwenye mizunguko..
Anza kubadilika kwanza wewe.. Tatizo sio dhehebu tatizo ni wewe.. Kumbuka Mungu haletwi na dhehebu analetwa na wewe.. MUNGU hayupo kwenye dhehebu yupo kwako wewe.. Wewe ndo wakufanya changes katika kanisa lako

📌Technology.. Utandawazi
Utandawazi ni mzuri sana ukitumiwa vile ipasavyo. Mfano sisi tunafundishana Neno kwa mtandao ambao ni matokeo ya utandawaz..
Lakini nikuthibitishie pia kuwa utandawazi ni njia pia shetan anatumia kupandikiza ufalme wake dunian.. Nowaday watu wanatumia simu au Internet kuangalia picha za ngono hasa vijana na zinaathiri moja kwa moja mifumo yao ya kufikiri.. Nowaday mtu yuko radhi asiende kanisan asisome biblia ila ata watch series.. Movie hata  masaa kumi na mbili.. Huo muda angekua ameutumia kusoma Neno au kufanya maombi na kufanya mambo ya kimsingi kama biashara etc agekuwa amepiga hatua..
Ngoja nikwambie mpendwa.. Muda ni mali.. Sababu maisha yako ni muda. Ikiwa  umeandikiwa kuishi miaka mia unapotoa masaa 12 kuwatch movie au kukaa online na kufanya mambo yasiyo ya msingi basi ujue umebakiza miaka tisin na tisa na siku 364 na nusu.
Unapotoa muda unatoa maisha yako.. Sasa huo muda unaotoa je unafanya mambo ya kukujenga au ndo siku ziende tu?
Kumbuka kila mtu atatoa hesabu ya matendo yake siku ya mwisho..  Na upo ujira kwa kila jambo..
✍Tumia utandawazi positively na sio negatively..
✍shetan ataendelea kubun vitu vipya kila wakati ili tu kukuchanganya.. Sasa usipokaa sawa katika Neno kunahatari ya kupelekeshwa na ulimwengu
✍ Hujaumbwa kupelekeshwa na ulimwengu umeumbwa kuupelekesha ulimwengu..
✍  utandawazi ni mzuri ukitumiwa kwa hofu ya ki Mungu ila utandawazi ni hatari ukitumiwa pasipo hofu ya Mungu

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA HIZI HAPA

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

ondoa jiwe iliujibiwe maombi yako