GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

SOMO: MWONGOZO WA KIBIBLIA WA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO

*2⃣ SOMO: MWONGOZO WA KIBIBLIA WA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO*

*ENEO: SINGIDA*

*SIKU: 2*

*MWL. C. MWAKASEGE*

*TAR: 5 JUNE 2017*

UTANGULIZI

MAOMBI.

Mungu uliye hai sifa na heshima ni za kwako kwasiku ya leo sawasawa na jinsi ulivyo kusudia Tuhudumie kwa jinsi inavyo kupendeza . Asante kwa kila mmoja ambaye umemfungua masikio ya nje na ya ndani ili apate kusikiliza neno lako siku ya leo. Nguvu zako na uweza wako uwe pamoja nasi eeh bwana kutujalia kupata kile ambacho umetujalia kupata  katika jina la Yesu Kristo  na watu wote tuseme ameeen!!!.

Bwana YESU Asifiwe!!!!

Somo letu ikiwa Leo ni siku ya pili lina kichwa kinacho sema MUONGOZO WA KIBIBLIA WA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO leo ni siku ya pili  maana yake tulianza jana kama siku ya kwanza na jana tulizungumzia juu ya gharama ambazo mtu anaweza kupata kwa kutokujua namna ya kutafsiri na kuombea ndoto kibiblia. Wakati tunangaalia ile ndoto ya farao ambayo ilikuwa inamwaarifu juu ya njaa iliyokuwa inakuja katika nchi na tukapitia vipengele kadha wa kadha kama hukuwepo hakikisha unapata kanda au CD ya jana.

Fuatilia pia tuna masomo mengine tuliyofundisha sehemu zingine, tulipokuwa Tanga tulijifunza pia juu ya ndoto lakini kutoka kwenye kona nyingine kwa hiyo unahitaji kufuatilia haya masomo yatakusaidia

Bwana YESU Asifiwe!!!.

LENGO LA SOMO

Lengo la la somo hili sio kujifunza juu ya ndoto, lengo la somo hili kwa njia ya somo hilo la ndoto uweze *kuimarisha uhusiano wako na MUNGU katika KRISTO YESU*, hilo ndilo lengo kubwa. Kwa sababu kama tutakufundisha habari za ndoto halafu uhusiano wako na MUNGU katika KRISTO usiimarike tutakuwa hatujafikia kile MUNGU anachotaka.

Si rahisi tukakueleza kila kitu kwa siku chache zilizoko lakini angalau vitu vya msingi vya kukusaidia katika kutafsiri hata usipo pata mtu mwingine wa kukusaidia lakini angalau vile vichache ambavyo unaweza kuvipata wewe wenyewe uweze kuvipata.

Nilikueleza jana mahangaiko niliyopata wakati MUNGU ananisemesha kwa njia ya ndoto miaka ya 80 pale mwanzoni akinisemesha  juu ya maisha yangu ya baadaye na utumishi alioniitia na sikuelewa na nikatafuta kutafuta msaada na kwenda mahali panapo stahili maana sikujua ntapata msaada wapi na kanisani hatukuwa na hayo mafundisho kabisa walawatu wa MUNGU niliokuwa nawafahamu ambao wanaweza nieleza juu ya ndoto kwa usahihi kwa hiyo nilienda kwa watu wa imani nyingine (waganga) akajitahidi kutafuta kunieleza kwa upande wa kwao na imani ya kwao maana alikuwa hana namna ya kunielekeza kwa Mungu katika Kristo Yesu, lakini namshukuru MUNGU aliyenishikilia ili nisizamie huko.

Ni rahisi sana ukavurugwa imani yako kwa kupitia kwenye ndoto au kufuatilia maana ya ndoto, na ndiyo maana ni vizuri sana upate mwongozo wa hatua kwa hatua kidogo

Hatua mojawapo ya KWANZA ambayo nataka tuingalie ni hii:

Omba MUNGU akupe ufahamu wake juu ya kutafsiri na kuombea ndoto

Na ukiweza hili ombi liwe ombi la kudumu kwako kadri unavyokumbuka muombe MUNGU hili jambo, tumia muda kuomba utashangaa kitu MUNGU atakacho kufahamisha juu ya kutafsiri na kuombea ndoto.

Daniel 1:17 “Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto”

Nataka uone hili neno…..”Daniel naye alikuwa na ufahamu katika maono na ndoto”….

Alivipata wapi? Biblia inasema MUNGU aliwapa maarifa, kwa hiyo MUNGU aliyewapa

Wale wenzake watatu walipata tu maarifa na ujuzi na elimu na hekima. Daniel alipata vyote hivyo pamoja na ufahamu katika maono yote na ndoto.

Msomaji wa Biblia katika Agano jipya anajua kabisa ni kati ya maombi ambayo ROHO MTAKATIFU  amekuwa akiyapeleka ndani ya watumishi mbalimbali kuomba juu ya ufahamu tuweze kupata ufahamu katika utu wetu wa ndani ufahamu unaofanana na yeye aliye tuumba…ndivyo Biblia inavyofundisha

Mwanzo  40:5-8 “Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.  Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie”

Yusufu aliwaambiwa ukweli kabisa ya kwamba kufasiri ndoto ni kazi ya MUNGU lakini MUNGU anawapa watu huo ufahamu…ndiyo maana aliposema kufasiri ni kazi ya MUNGU niambieni mimi, kwa lugha nyingine alikuwa anawaambia MUNGU amenipa ufahamu, amenipa uwezo wa kufasiri ndoto. Si mimi ninaye fasiri lakini MUNGU ameweka uweza ndani yangu.

Kwa hiyo kama MUNGU aliweza kumsaidia Yusufu, aliweza kumsaidia Daniel nani  katika Agano la kale agano ambalo halilingani kiubora na Agano tulilomo sasa, Agano tulilonalo ni Agano jipya ni bora zaidi kulikuwa agano la kale limeahidiwa katika ahadi  zilizobora zaidi tunaye kuhani Mkuu mfano wa Melkizedeki ambaye hafi tena alikufa na kufufuka.

Biblia inazungumza ya kwamba ahadi zilizoko katika Agano jipya ni bora zaidi kuliko zile za agano la kale, Biblia inazungumza ya kwamba ROHO MTAKATIFU katika Agano jipya situ anakuja juu ya mtu lakini anakaa ndani tena si kukaa ndani mara moja anakaa naye siku zote

Kwa hiyo kama MUNGU aliweza kuwapa ufahamu katika agano la kale si zaidi sana anaweza kutupa pia ufahamu katika agano jipya. Unahitaji kufikiri sana kwa namna hiyo ilikuweza kuona kwa sababu ni rahisi sana ukasema wale walikuwa ni watumishi wa MUNGU, wale walikuwa watu wa MUNGU kwa hiyo MUNGU aliwapa wao peke yao…Lakini ukisoma kile kitabu cha Ayubu 33:14-15 unaweza kuona kitu tofauti kidogo

Ayubu 33:14-15 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani”

Hapa hazungumzii juu ya watumishi wala cheo cha mtu bali anazungumza juu ya mtu. Ndoto ni njia mojawapo ambayo MUNGU anazungumza na mtu, na MUNGU anapotaka kuzungumza na wewe anataka usikie la sivyo hakuna sababu ya kuzungumza na wewe, anataka usikie na ndiyo maana anarudi mara ya pili hata kama hujadaka au hujali anachokusemesha kwa sababu yeye anajali usikie anachokuambia anakirudisha tena na kukirudisha tena, na njia mojawapo anayoitumia ni ndoto.

Kwa hiyo kama MUNGU anataka tumsikie anaposema na sisi kwa njia ya ndoto uwe na uhakika atataka kutupa na ufahamu na uweza wa kuweza kusikia.

Sasa kama MUNGU anataka kwa kiu namna hiyo kwanini tuombe basi si atupe tu?

Lakini kama unasoma Biblia utajua ya kwamba dhambi ilipoingia katika bustani ya Eden ilituvurugia mambo mengi sana

ilimwondoa MUNGU katikati yetu katika ule uhuru wa kiushirika,

ikaondoa sura ya MUNGU ndani yetu

Ikaondoa mfumo wake wa UFALME

Ikatuondolea hali ya mawasiliano na MUNGU

Biblia inasema dhambi zetu zimetutenga na uso wa MUNGU na mkono wa MUNGU. Kumekuwa na kitu kimekatika na tangu wakati huo mwanadamu akihitaji msaada wa MUNGU lazima apelike ombi kwa sababu mwanadamu alimkataa rasmi.

Kabla ya dhambi haijakuwepo hakukuwa na maombi ya stahili hii kulikuwa na fellowship (kulikuwa na ushirika). MUNGU alikuwa anakuja kwenye bustani kukaa na wewe kuzungumza na wewe kulikuwa na uwezo wa mwanadamu kuishi katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa kimwili kwa wakati mmoja bila kuogopa juu ya mauti, mauti haikuwepo mauti imekuja kwa sababu ya dhambi ilipoingia, dhambi ilipoingia ilileta mauti Biblia inasema kwa hiyo kufa hakukuwepo mwanadamu alitakiwa kuishi milele akiwa na mwili wake,roho yake na nafsi yake ndiyo mpango wa MUNGU ulivyokuwa mpaka dhambi ilipoingia, dhambi ilipoingia ikaurubuni mwili, mwili hautaki tena kuurithi UFALME WA MUNGU ndiyo maana damu na nyama haviwezi kuurithi tena UFALME WA MUNGU ndani yake kuna mbegu ya uasi ambayo inasumbua mpaka leo.

Ndiyo maana MUNGU alituletea plan B, ambayo inaitwa Adamu wa mwisho ili tuweze kutembea ndani yake na ndani yake tunapewa mwili mpya, tunapewa na roho mpya, tunahuishwa nafsi zetu ili sasa pia tuweze kufika katika kile kiwango alichokikusudia na ndiyo maana inapofika katika mazingira  ya namna hiyo swala la kuomba liko pale. Ndiyo maaana hata kama MUNGU anajua una uhitaji usipoomba saa nyingine hakupi ndivyo Biblia inavyosema….”hampati kwa sababu hamwombi na mkiaomba mnaomba vibaya”…

Swala la kuomba ni swala la wewe kufahamu nafasi ya MUNGU kwako ni swala la wewe kufahamu mahusiano yako na MUNGU ni swala la wewe kujua Biblia inasemaje.

Kwa hiyo swala la kuomba ufahamu juu ya mambo mbalimbali ya KIMUNGU ni agenda ya msingi kubwa itakusaidia katika kutazama vitu mbalimbali kwa picha ya MUNGU, kwa sura la MUNGU kwa tafsiri ya MUNGU siyo kwa tafsiri ya watu , wala yako wala ya watu Fulani fulani lakini utaenda kwa tafsiri ya MUNGU na itakufikisha mahali pazuri sana

Kwa mfano unapoenda kwa ajili ya kuomba ufahamu juu ya ndoto kuna vipengele vingi sana ndani yake lakini ninachosukumwa kukueleza ni:-

Kuomba MUNGU akupe ufahamu wa KIMUNGU wa kuunganisha unachowaza na unachoota.

kibiblia kuna muunganiko Fulani kati ya unachowaza na unachoota

Wale ambao wanakumbuka jana tulipokuwa tunazungumza Daniel 2:16 wasomaji wa Biblia wanajua mahali ilikotoka kwamba Nebukadreza aliota ndoto akasahau akaita wachawi, waganga na wenye hekima wakaridayo wa wakati ule ili kwamba wamsaidie kutafsiri ndoto tatizo ni kwamba alikuwa amesahau ile ndoto lakini yeye aling’ang’a kwamba wamwambie ndoto aliyo isahau na tafsiri yake la sivyo atawaangamiza na wale waganga wakasema si kitu sisi tunaweza kufanya ni lazima watu wenye roho ya miungu ndani yao ndiyo wanaweza. Kwa lugha nyingine walikuwa wanakiri kwamba swala la ndoto limezidi kiwango cha kwetu kuna vipengele tunaweza kubaatisha lakini hapo lilipo hatuwezi kuingia hapo tafuta watu wenye roho ya miungu ndani maana yake ni kwamba walizungumza kwa lugha yao,  maana yake tafuta mtu mwenye ROHO wa MUNGU maana yake MUNGU ameweka hicho kitu ndani. Na katika kumpa kiongozi wake atoe hiyo adhabu kwa wale wenye hekima kina Daniel walikuwa kwenye kundi la wenye hekima ingawa hawakuitwa mbele za mfalme lakini adhabu ikawafikia na wao na ule mstari wa Daniel 2:16-18 “Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli.” Ukiendelea unaona ya kwamba Daniel baada ya maombi yale alifunuliwa ndoto ya Nebukadreza  ambayo Nebukadreza ameisahau na akapewa tafsiri na kapewa na ujumbe ndani yake.

Sasa tuangalie Daniel 2:26-30 “Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake. Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu; lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi; Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa. Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako.”

Huyu ni Daniel  anamweleza Nebukadreza ili asimtazame kama vile yeye ni mmojawapo ya waganga amtazame kama vile ni mmoja wa wawakilishi wa MUNGU amebeba ufahamu wa MUNGU na kwamba anamrudishia MUNGU heshima na shukrani kwa kumpa nafasi ya kujua hayo mambo ndiyo maana alimwambia pale kwamba yupo MUNGU mbinguni afunuaye siri.

30…..nawe upate kujua mawazo ya moyo wako… maana yake MUNGU amekuja kukusemesha juu ya kitu kilichoko ndani ya moyo wako. Inawezekana hajazungumza na mtu, akumweleza hata na mkewe wala watu wake lakini amelala akiwaza

Mathayo 1:18-24 “Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,  Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.  Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;”

kitu gani hii ndoto ilikuja kufanya?? Kujibu kujibu maswali na mawazo na maamuzi yaliyokuwa ndani ya Yusufu wakati analala, lilikuwa linamsumbua anafanyaje baada ya kupata taarifa kwamba mchumba wake ni mjamzito na lazima huku mjini walishaanza kusema Yusufu kampa mimba msichana wa watu kabla ya harusi rasmi. Lazima maneno yalikuwa yanapita mtaani, Yusufu alijua mimba si ya kwake Mariam alijua mimba si ya kwake, Mariam hana namna ya kuwambia ndugu zake na majirani na marafiki waliojiandaa kwa harusi kwamba malaika alinitembelea hata akiwaambia kuamini kwao kunaweza kukawa na shida. Yusufu hakukuwa na namna ambavyo angeweza kuzungumza na wenzake jinsi walivyokuwa wamekaa mkao wa kuoana na Mariam anajikung’utaje ya kwamba mimba si yak wake anafanyajefanyaje..lakini Yusufu alienda mbali kidogo kwanza kwamba akikataa mzigo wote wa lawama  na hasira za watu zinaishia kwa Mariam. Na akataka kumsaidia kuubeba ule mzigo Biblia inasema…akahazimu kumwacha kwa siri…. Ili atakapotoroka waseme kama hawakuwa na shida kwanini ametoroka kwa hiyo atakuwa amebeba mzigo wa lawama ili kumtua Mariam ule mzigo akifikiri kufanya namna hiyo anafanya sawa.

Biblia inasema alikuwa nafikiria namna hiyo na ni usiku ghafla amelala malaika akamtokea kwenye ndoto akamweleza kilichotokea. Kwanini? Kwa sababu hata kama Mariam alimwambia Yusufu kilichotokea hakuamini kwa hiyo ilibidi malaika aje kumweleza kwenye ndoto na ile ndoto haikuwa na fumbo la aina yoyote ilikuwa na maagizo na maelekezo sahihi

Yusufu alipoota ile ndoto ndani yake MUNGU aliweka na ufahamu. Saa nyingine ndoto inapokuja inakuja ikiwa imebeba ufahamu ili kumfahamisha yule anayeota kilichoko. Sasa kwa sababu si watu wengi sana hawajajifunza kupokea ufahamu au kuomba ufahamu au kukaa mkao wa kupata ufahamu hawaoni umuhimu wa kutafuta mbele za BWANA ufahamu

Hii ni sawasawa na mtu ambaye yuko darasani ambaye anataka kusoma lakini hataki kufahamu anachosoma, anaweza kufaulu mtihani lakini atafeli maisha kwa sababu maisha inatakiwa upate ufahamu Biblia inazungumza na kutuambia ufahamu unaenda na maarifa, unaweza ukawa na elimu usiwe na maarifa, unaweza ukawa na elimu usiwe na ufahamu. Unaweza ukaenda  kanisani ukasikiliza mahubiri wewe ulichoenda kanisani ni kusikiliza mahubiri hujatafuta ufahamu ndani yayale mahubiri kwa hiyo utatoka ukitueleza mahubiri uliyosikia mwingine atatoka kutueleza ufahamu alioupata kutoka kwenye yale mahubiri na ni vitu viwili tofauti.

Yule aliyepata ufahamu atakuwa mwepesi kuweka kwenye matendo kipengele kile alichopata ufahamu atakueleza mahubiri yote yaliyokuwepo lakini kile alichopata ufahamu ndicho atakachokifanyika kazi maana ndicho kinachoachilia imani yake ndani yake, ndicho kinachomfungua na kumsaidia aweze kuona lile jambo kwa sura la yule ambaye anamfundisha

Sasa turudi kwa Yusufu…Yusufu alipata ufahamu gani?? Ngoja nikutajie baadhi ya ufahamu uweze kuelewa mahali tunapoelekea

1. Ndoto ile lilikuwa jambo la halisi lililokuwa linatokea wakati ule ule alipokuwa anaota ndoto

…sababu kuna ndoto zingine zinakuletea mambo yaliyopita kwa hiyo ni kama inachokua rekodi mahali inapiga ndani yako au picha inacheza ndani yako au inaenda kwa vitu vya mbele inakuletea vitu vya mbele inakuletea sasa kukueleza vitu vya mbele lakini pia saa nyingine inakuletea vitu vinavyotokea katika ulimwengu saa hiyo hiyo…unasema unajuaje?....kwa sababu Biblia inasema alipoamka alitekeleza alichoambiwa saa ile ile

2. Alipata ufahamu ya kuwa MUNGU alikuwa anajibu maamuzi yake aliyokuwa nayo juu ya kumuoa au kutokumuoa Mariam

Yeye Biblia inatuambia alishafanya uamuzi kumuoa au kutokumuoa, Biblia inaseme yeye alishafanya maamuzi ya kumuacha Mariam kwa siri, kwa hiyo inamaanisha ilikuwa siri yake. Hakuna watu wengine walikuwa wanajua bali yeye peke yake, Majirani zake hawajui, best man wa Yusufu hajui, ndugu zake hawajui, wapambe hawajui, kamati ya maandalizi hawajui,wachangiaji wa harusi hawajui kaamua kumuacha kimya kimya. sasa rudi kwenye kitabu cha..

Ayubu 33:14-18 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;  Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,  Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi;  Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga”

16…..ndipo uyafunua masikio ya watu…maana yake anatafuta usikie, kama ulikuwa si msikivu au MUNGU amekutumia watu kwa njia mbalimbali bado atakuja kufunua masikio ya ndani lakini la pili …kuyatia muhuri mafundisho yako… maana yake ni kwamba kama ni mafundisho ambayo unajisikia  kusita kama kuna jambo unasikia kusita na jambo hilo ni sahihi kwa njia ya ndoto MUNGU anaweza akaja akalipiga muhuri kukuhakikishia ya kwamba ni la kwake ni sahihi

17…ili kumwondoa mtu katika mafundisho yake…ili kumwondoa mtu katika makusudio yake…Maana yake ni kwamba njia mojawapo ambayo MUNGU anaitumia kuja kupangua kitu ulichokikusudia ndani yako ambacho hakikosawa na mapenzi ya MUNGU kwa ajili yako njia mojawapo atakuja kwa njia ya ndoto kupangua makusudio yako, nia yako..Biblia inaendelea kusema na kumfichia mtu kiburi…Biblia inasema yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni..kwa kukusaidia namna hiyo anazuia nafsi yako isiende shimoni na uhai wake usiangamie kwa upanga

Kwanini nimekusomea namna hiyo….Huyu ndugu amekusudia kumwacha Mariam kwa jinsi ya kibinadamu ulikuwa uamuzi sahihi kwa jinsi yake na huduma Biblia inasema kwa jinsi alivyokuwa mwenye haki akaazimu kumwacha Mariam kwa siri ili abebe mzigo wa matukano na matusi kwa Mariam lakini MUNGU alikuwa anamipango mikubwa zaidi kuliko hiyo, alikuwa na njia ya kuwasaidia wakiwa pamoja kuliko wakiwa tofauti na kwasabau hiyo alitumia ile njia kupangua makusudio yake ya kumwacha Mariam na ule ufahamu aliupata alipokuwa anaota, iliingia moja kwa moja kwamba MUNGU ananisememsha jambo hili. sasa kama umeanza kuomba kuwa “Mungu naomba nisaidie au nipe ufahamu juu ya kuunganisha ndoto ninayoota na vitu ninavyowaza utashangaa vitu ambavyo Mungu atakuwa anakusemesha.

3. Alipata ufahamu saa hiyo hiyo ya kwamba atii alicho ambiwa kufanya ndani ya ndoto

Asinge pata huo ufahamu angetafuta kwanza mganga kama wengine tulivyokuwa tunatafuta kwenda kuuliza.

Asinge pata huo ufahamu unatafuta kuwaeleza wapendwa wawili watatu wanane kwamba umeota ndoto unachotafuta ni msaada wa kupata ufahamu wa kilichoko ndani yeye alipata ufahamu saa hiyo hiyo moja kwa moja na alipo amka akatii saa hiyo hiyo

Angeweza akachelewa hatuwezi kujua gharama yake ingekuwaje,  Jana nilikupa mfano wa mtu ambaye aliota ndoto kuwa pochi yake (wallet) imeibiwa na kufika ofisini kesho yake, kazi aliyokuwa nayo  imepotea lakini angeweza kujua kutafsiri  ndoto na kuomba ninapofundisha juu ya ndoto nafundisha pia juu ya muda ulioko ndani ya ndoto kwa sababu MUNGU anakupa huo ufahamu wa ndoto

Unasema unajuaje? Kamuulize Yusufu atakwambia alijuaje ya kwamba zile ndoto za muokoaji na nyweshaji zina siku tatu tatu, hakukuwa na mahali pameandikwa tatu lakini kulikuwa na vitu vimekaa vitatu vitatu, kwanini aone ni siku tatu na si miezi  mitatu? Lakini alipata ufahamu kwamba hizo ni siku tatu, maana yake walikuwa na siku tatu ya kujipanga au kupangua kilichoko. Yule aliyeota ndoto ile ya kuibiwa pochi (wallet) alikuwa na masaa machache tu .

Ingawa si kila ndoto inajibu juu ya unachowaza kinachohusu baadaye yako lakini ukiweza kuomba ni vyema sana MUNGU akakupa huo ufahamu tayari ili siku atakapoamua kusema na wewe kwa njia ya ndoto maana ni uamuzi wa MUNGU sio lazima umlazimishe kwamba sema na mimi kwa njia ya ndoto ana njia nyingi za kuzungumza na watu hii ni njia mojawapo tu..siku atakapoamua kusema na wewe kwa njia ya ndoto uwe na ufahamu tayari ndani hata kama ni vitu vichache uvivahamu basi viwe ni vitu vichache lakini vingine uweze kupata ili kama ni jambo ambalo unahitaji kulifanyia kazi mara moja uweze kulifanyia kazi mara moja kwa sababu la sivyo unaweza kukwama kimaisha, unaweza kuvurugwa kimaisha kabisa, unaweza ukapoteza kile MUNGU anachotaka ufanye, unaweza usitembee katika makusudi ya MUNGU, unaweza usijue MUNGU anataka nini kesho au kesho kutwa, unaweza usijue MUNGU anakuandaa kwa ajili ya kitu gani baadae

Ukipata ufahamu mapema itakusaidia kama si kwa ajili yako basi kwa ajili ya watu wengine ambao wanaweza wakawa wanakuja kuzungumza na wewe na kukueleza ndoto walizoota utapata ufahamu na kama ufahamu hujaupata saa hiyo hiyo uwe na ujasiri na hekima na unyenyekevu wa KIMUNGU usijifanye mjuaji sema ngoja nikaombe hakuna hasara hata Daniel alimwambia Nebukadreza nipe muda nikaombe kwa sababu si yeye anaye tafsiri ni MUNGU. MUNGU akikupa ufahamu saa hiyo hiyo kama Yusufu alivyopewa unaweza ukasema na ukamsaidia na yule mtu mwingine

Ninachotamani ndani upate hiyo kiu sababu ninajua ya kwamba si watu wengi sana wanaomba vya kutosha ni kwa sababu hawajajua gharama iliyoko. MUNGU amenipa nafasi ya kusoma ndoto za watu wengi sana na kila ninaposoma inanisumbua sababu watu wengi sana maisha yao yamekwama kwa sababu hawana ufahamu wa MUNGU juu ya ndoto hawana ufahamu wa Kibiblia  juu ya ndoto na kwa sababu hiyo maisha yao yamekwama na yamekwama vibaya

Kwa wale ambao wanaweza kuingia kwenye ukurasa wa facebook ingia kwenye ukurasa wetu wa facebook Christopher and Diana Mwakasege (MANA Ministry)  au bonyeza hii link    https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/  nimekuwa nikifundisha somo la ndoto kwa mfululizo sasa yatakuwa yamefika msomo 12 au 13, kila nikitaka kuacha niweke somo lingine ROHO MTAKATIFU anasema andika na hiki andika na hiki, ukienda kule ndani masomo yote bado yapo hatuyaondoa kasome moja baada ya jingine utaona kilichoko.

Tuingie ndani kidogo kwa mifano juu ya KUANGALIA kibiblia NA NAMNA YA KUOMBA kibiblia JUU YA TAFSIRI ZA NDOTO LAKINI ZINAZOHUSU KUOA AU KUOLEWA AU NDOA kwanini?

Kwa sababu katika swala la Yusufu huyu Yusufu aliyemuoa Mariam unaona kabisa MUNGU alitumia ndoto kusema naye juu ya maamuzi yake ya kuoa au kutokuoa juu ya maamuzi yake juu ya ndoa yake. Na MUNGU mpaka leo anazungumza na watu wengi sana juu ya kuoa au kuolewa na juu ya ndoa zao kwa njia ya ndoto na ibilisi naye anatafuta kila mbinu ya kupitisha mashambulizi yake kwenye lango hilo kwa makusudi kabisa kwa sababu anajua ni watu wachache sana  wanajua namna ya kumpangua akipita kwenye hilo lango

Nikupitishe kidogo kwenye mistari uweze kuelewa kwa mifano kufuatana na jinsi ambavyo ROHO MTAKATIFU alivyokuwa ananipa…

1. Cheki ndani yako unachowaza juu ya kuolewa kwako (kama hujaolewa) juu ya kuoa kwako (kama kijana hujaoa) au cheki unachowaza juu ya hali ya ndoa yako (kama uko ndani ya ndoa) cheki kwanza hicho juu ya maswali uliyonayo, maamuzi uliyonayo cheki..halafu ghafla  MUNGU ataanza kukupeleka au kwenye ndoto ambazo ulizoota na hukujua au MUNGU atakuletea ndoto nyingine ambazo zitazungumza na wewe moja kwa moja kweupe

Mfano:

Ndoto: Ukiota unafunga ndoa na mtu uwe unamjua au humjui halafu baada ya kuamka ukakosa amani na kufadhaika maana yake nini?

Maana: MUNGU anataka ujue na anakujulisha ya kwamba hiyo siyo ya kwake ila kuna roho au kuna pepo linaloambatana na wewe kama mwezi wake wa maisha kindoa wala halina mpango wa kukuachia kwa hiari yake..unasema unaipata wapi? Kwenye kitabu cha Marko

Marko10:7-9 “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”

Kumbuka hili jambo linapozungumzwa halizungumzwi kwa jinsi ya m wili kwanza linazungumzwa kwa jinsi ya rohoni kwanza.

Ndoa inafanya watu wana ambatana, kuambatana maana yake ni kufuatana kimuunganiko hamfuatani tu mnafuatana kwa sababu mmeunganika.Sasa katika ulimwengu wa roho pepo linaweza likaja kufuatana na mazingira mbalimbali yaliyoko na ndiyo maana unapoota ndoto za namna hiyo cheki hiyo ndoa imefungiwa wapi, kama imefungiwa makaburini ina maanisha kuna roho ya kuzimu au ya kimila inatafuta namna ya kukujulisha ya kwamba nafsi yako imeambatanishwa na sisi kwa hiyo huwezi kuolewa au kuoa bila kibali chetu, hatuna mpango wa kukuachia na ndiyo maana wengine wanapojua vitu vya namna hiyo wanakwambia lazima uende kwa babu au bibi yako aliyekufa akupe kibali cha kuolewa ama kuoa…ukisikia namna hiyo ujue tayari umeshafungwa kindoa na roho ya kuzimu utakaa kwenye hiyo ndoa au utaolewa kwa masharti..na kwa sababu kuolewa ama kuoa kwako kunaweza kukawa na shida na ndoa ikawa na shida.

Ukianza kuota ndoto za namna hiyo na unasikia ROHO MTAKATIFU akikuwekea ile hali ya kukukosesha amani na kukufadhaisha ndani ni ishara ndani yake.

Na ndiyo maana saa nyingine unapoota ndoto za namna hii cheki waliokuja kama mashahidi ni watu wa namna gani..unakuta unafunga ndoa na woote walikuja hapo wamekufa. Unajua kabisa hii si ndoa ambayo imekaa sawa sasa katika ulimwengu wa roho usije ukahidharau hii ni ndoto tu..katika ulimwengu wa roho unajulishwa kuna roho ilioambatana na wewe kindoa na inaweza kukuvuruga kabisa

Unakuta msichana mwingine anabaki anashangaa anabaki anashangaa anakaa anawaza kwanini mchumba mwingine ameniacha na yule ameniacha..usiku anaota ndoto anafunga ndoa na hajajua ya kwamba MUNGU anajaribu kumsemesha kwamba umefungwa msichana unahitaji kupangua kwanza hiyo ndoa katika ulimwengu wa roho ili upate hii ndoa nyingine

Au umekaa kwenye ndoa unashangaa ndoa haikai sawasawa unakaa na kung’ang’ana na MUNGU nimekosea wapi, usiku unaota ndoto unafunga ndoa na mtu mwingine MUNGUanajaribu kukusemesha kwamba kuna roho nyingine iliyoambatana na wewe ilitangulia kabla yah ii ndoa na ina msharti ya kwake na inakuvuruga na kwa vijana hivyo hivyo

Ndoto: Ukiota unazini na mtu kwenye ndoto

Maana: Soma Mithali 6:26,32-33, “  Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani   Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.  Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.”  1 Wakorintho 6:16  “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja”.

Kama unaota unazini na mtu kwenye ndoto mistari iko mingi kwenye Biblia nimeona nikuonyeshe kidogo ili iweze kukusaidia namna ya kutafsiri ndoto kibiblia, ROHO MTAKATIFU atakuongoza kujua ya kwako inahusu mstari upi na ndiyo maana ya kuomba ufahamu lakini unaona kabisa kibiblia kama unazini na mtu kwenye ndoto shetani anawinda nafsi yako na anawinda mwili wako

Na Biblia inazungumza wazi kabisa ukiendelea na mistari tofauti tofauti Biblia inasema anaye ambatana na kahaba hutapanya mali, kwahiyo ukishaona unazini kwenye ndoto cheki matumizi yako ya pesa baada ya kuota zile ndoto au wakati unaota hizo ndoto inawezekana unajiuliza kwanini pesa haikai mkononi najitahidi MUNGU nafanya kazi nafanya biashara pesa inakuja lakini nashangaa pesa haikai hata kitu ninachofanyia hakionekani ghafla  usiku unaota ndoto unazini na mtu. Sasa kwa sababu huna ufahamu wa kuunganisha unachowaza na unachoota ni vigumu sana kuunganisha kutawanya pesa na kuzini kwenye ndoto lakini Biblia imeandika

Kuzini kwenye ndoto shetani anawinda kitu gani? Ni kuvuruga akili zako…aziniye na mwanamke hana akili….siyo kwamba hana ubongo bali hana akili maana yake inavuruga kufikiri kwako na matokeo yake unaweza kujikuta pesa hazikai, kuolewa kwako au kuoa ni shida, kukaa kwenye ndoa ni shida ndoa inavurugika kwa chuki isiyokuwa ya kawaida kwanini kwa sababu kama unazini kwenye ndoto inamaamnisha ile roho iliyoko kwenye ndoto inawivu na huyu aliyeko kwenye mwili unajikuta unamchukia tu pasipo sababu tu na hauna sababu.

Ndoto: Mwingine akiniandikia akisema Mwalimu nahitaji msaada niliota kuwa niko uchi na nilienda kwenye banda la ng’ombe na ng’ombe  amezini na mimi., Mwingine aliota anakimbizwa na simba mwishoni akachoka yule simba akazini naye sasa maana yake nini hizi ndoto

Maana: Kutoka 22:19, “Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.” Mambo ya Walawi 18:23 “ Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.”  Ndoto za namna hii shetani inapandikiza roho ya mauti kwako, kunajisika na kuchafuka na kukataliwa kwa hiyo kuna vitu kwenye maisha yako vitaanza kufa kidogo kidogo ni mbegu imepandikizwa kwa njia ya ndoto na inawezekana saa nyingine umekuwa ukiomba MUNGU kwa nini vitu vyangu naanzisha vinakufa gafla unaota ndoto za namna hii

Ndoto: Mwingine ameota ndoto amezini na mtoto wake wa kiume

Maana: Mambo ya Walawi 20:17,19-21  “Tena mtu mume akimwoa umbu lake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume; ni jambo la aibu; watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa umbu lake; naye atauchukua uovu wake. Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao. Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.”

“MUNGU anajaribu kukusemesha kwa njia ya ndoto kwamba moja umefungulia roho ya uovu, roho ya uovu ndiyo inayopatilizwa toka kizazi kwenda kizazi kingine, ina maanisha adui anatafuta mlango wa kutoa nafasi ya adhabu kutoka kizazi kimoja kuingia kizazi cha kwenu. Biblia haizungumzii juu ya dhambi hapa inazungumzia juu ya uovu.

Uovu ni udhaifu unaotoka na unatokana na uasi ulioko katika eneo fulani na MUNGU anapatiliza uovu hapatilizi dhambi, kila mtu atakufa kwa dhambi yake lakini uovu unaenda kizazi mpaka kizazi cha nne cha watu wamchukiao.. lakini Biblia inazungumza ya kwamba atakataliwa kwa hiyo inatumbukiza roho ya kukataliwa (spirit of rejection) na pia mbegu nyigine ya kuharibu uzazi wa hao watu, watakuwa hawana watu hiyo ni laana. Nimekutana na ndoto za namna hiyo nyingi na siwezi nikamjibu kila mtu. kwa hiyo ninapo pata nafasi ya namna hii huwa namuuliza Mungu ni ndoto za namna gani unataka niwajibu watoto wako. Angalau uwape mtaji mahali pa kuanzia. Ndoto za namna hiyo ziko nyingi na watu wanaandika vitu vigumu sana.  Sasa ukiota ndoto za namna hiyo suala la kuolewa linakuwa gumu sana.

Ukiweza kuvuka kwenye kuoa au kuolewa, kukaa kwenye ndoa na ndoa ikawa na raha ni shida kubwa kwa sababu lazima ujue si tu kutafsiri zile ndoto zinazokueleza mambo yaliyoko lakini pia upate ufahamu wa mambo yaliyoko lakini pia upate ufahamuwa namna ya kuombea kibiblia jambo hilo

Mtu mmoja alikuwa ananieleza tatizo liloko kwenye ndoa yake  na saa hiyo ananieleza yuko na mke wake, mke wake amaepata shida ya kwake na baba naye amepata shida ya kwake vitu ambavyo siwezi kuvisema hapa. Wanapendana sana ila shida ndoa yao imekuwa ngumu sana  hawajapata hata mtoto. Mungu alinipa ufahamu  na nikazungumza na yule baba vitu vya kwao  na akanisikiliza hadi mwisho na alinikubalia hadi kiwango fulani na eneo fulani alisita. Basi nikamwambia tumuombe Mungu kwa kiwango tulichofika  baada ya siku kadhaa akaniandikia kuwa ameota ndoto mkononi mwake kwenye kidole cha pete ya harusi kuna pete juu yak wake ile aliyepewa na mke wake kuna juu ya kwake ndani ya nyama ya kidole akaona pete tatu zimefunikwa na nyama na juu yake ndo pete ya  nne ya mke wake (yaani ndoa ya sasa na ya mke wake ndio iko pete ya nne). Je hiyo pete ya tatu imetoka wapi?  na aliponiandikia hivyo nilielewa maana yake nini. Kasome biblia yako

Maana: Esta 8:2,8, “Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani. Basi waandikieni Wayahudi pia vyo vyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie muhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme hakuna awezaye kulitangua”  Yakobo 2:1-4. “Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?”

Pete ni alama ya agano haikuanzia Katika ulimwengu wa kimwili ilianzia katika ulimwengu wa kiroho ni alama ya agano, la lile agano linafuatana na nafasi. Ukipewa pete unapewa nafasi ya upendeleo unapewa nafasi ya kutawala. Hamani alinyang’anywa pete akampa Esta, Esta akampa Modekai kwa sababu ya ile pete akawa na mamlaka juu ya malango wa hamani.

Biblia inazungumza kwenye kitabu ya Yakobo kwamba kuna watu wanakuja na pete ya dhahabu ile pete ya dhahabu inaonyesha heshima anayopewa, gafla kwa sababu ya jinsi alivyovaa ile pete anapata heshima anaingia mahali anapewa mahali pa kukaa. Na ndivyo ilivyo hata leo ukivaa pete kuna heshima unayopewa situ katika ulimwengu wa kimwili katika ulimwengu wa kiroho inaweka alama.

Sasa kama kama katika ulimwengu wa roho kuna ndoa kuna maagano au ya kifalme, unaposoma Biblia maagano ya kifalme maana yake ni maagano yaliyoko katika ulimwengu wa roho na watu wanaotawala katika familia katika kabila katika eneo fulani fulani na ndiyo maana hutaona mahali popote mfalme akichaguliwa, mfalme anateuliwa na roho inayotawala kwenye eneo na ndiyo maana ufalme unaenda kwa kurithishwa

Tunapokuwa ndani ya KRISTO YESU anapokuwa MFALME anatufanya sisi tuwe wafalme hatuchaguliwi mahali tunarithishwa katika DAMU YA YESU ili tuwe tuwe wafalme ndani ya KRISTO na upande mwingine ni hivyohivyo

Sasa kama umeweka pete ya kawaida na ndani kuna pete zingine 3 maana yake kuna maagano tayari ya kindoa matatu unapoleta hii nyingine ya juu ni ya nne sasa usije ukafikiri haya maagano ya kwanza yatakuruhusu upate nafasi ambayo wao wamepata, kwa hiyo hutapata heshima unayostahili, hutapata kupendelewa, hutaheshimika, hutakubalika, hutapata nafasi ya kutawala. Unapete sawa lakini heshima yako kama mke au mme haipo, unabaki kujiuliza unapoanza kuomba MUNGU anakuonyesha kwenye  ndoto pete zingine ulizovaa au  unaona pete uliyokuwa umevaa imepotea

Ndoto: Wengine wanaota pete imepotea kwenye ndoto akiamka haipo kidoleni

Maana: Umenyang’anywa heshima yako uliyopewa na uwe na uhakika kwamba usipojua kuomba hiyo ndoa baada ya muda tu itaanza kuapata shida kama ilikuwa ni pete ya uchumba ukuipoteza namna hiyo uwe na uhakika huyo mwanaume au mwanamke atapotea na hautajua ni kitu gani kimetoke

Ndoto: Mwingine aliota pete ya ndoa imekatika

Maana: Usipoweza kuomba vizuri ndoa hiyo itakatika muda si mrefu ( Kwa sababu itakatika usipoomba)

Leo ngoja niishie hapa kesho tutapata nafasi ya kuingia ndani kidogo halafu nikueleza namna ya kuomba halafu tutaomba pia kwa watu wenye shida ya namna hii ili MUNGU angalau akupe mtaji ufunguke jumla lakini pia nitakupa hatua za namna ya kuomba na vitu vingi ambavyo MUNGU amenipa kwa ajili ya kuzunguza na wewe uweze kuelewa

Ndoto: Kuna mtu mwingine aliumwa na nyoka kwenye kidole chake cha pete na ndoa yake haikukaa amekuja kushtuka nilipoanza kufundisha akasema natamani ningejua hivi vitu mapema ndoa yangu isingepata shida

Nataka kuomba kwa ajili yako MUNGU akupe ufahamu wa ndoto kama una kiu ya kuona MUNGU anakupa ufahamu nataka niombe kwa ajili yako MUNGU akusaidie upate ufahamu kuna ufahamu wa aina tofautitofauti juu ya ndoto na mmoja wapo ni huu wa kuunganisha unachowaza na unachoota au unachoota na unachowaza, nimekuonyesha kwa jinsi ya Biblia angalau kwa uchache ili ndani yako kuwe na kiu usije ukafikiri ni kitu chepesi saa ingine ninawaza ROHO MATAKATIFU ananiambia waambiwe wenye ndoto zao waandike nimenyaza kimnya kwasababu nina bulungutu la ndoto ninazisoma kadri ninavyopata nafasi na vitu ninavyokutana navyo vinaweka mzigo mkubwa mzito, unatamani hawa watu wangejua gafla ili angalau waweze kujifungua wao wenyewewaweze kutoka kwenye shida waliyonayo. unaona waangamia kwa sababu hawajajua namna ya kutoka. sikuambii najua kila kitu. miaka ile ya 80 suala la ndoto lilinitesa nikaenda pole pole kwenye biblia na nikajifunza  kuomba ufahamu na asante Yesu kuna vitu ananipa kufahamu. usije ukafikiri ni vyepesi kuviombea  lakini angalau unaona kilichoko na inakusaidia kuweza kuzungumza na mtu mwingine.

Biblia inatuambia neema ya MUNGU inafundisha si tu inaokoa

wimbo wa neema ya Mungu…..

MAOMBI

Mungu uliyehai tunakuinulia mikono tukisema neema yako ni kubwa. Yanaonekana  ni mambo ya kawaida ee Bwana unaposoma au ukisikiliza watu wanaposema wameota ndoto  lakini kibiblia ni mambo mazito  yanaacha alama kubwa katika maisha yetu ya kiroho na katika jamii zetu bila kujua ya kwamba yameacha alama ya namna hiyo. na saa nyingine yanaachilia alama ambayo si rahisi kuifuta  Ee Mungu katika jina la Yesu  ni neema ilioje ee Bwana umetuokoa lakini umeamua kutufundisha , bado umeamua kutufunilia  neema yako ee Bwana inaokoa na inafundisha na  inafunua kile kilichokuwa kimefichwa. ee Bwana umeamua kusema nasi kwa njia ya ndoto nami ninaomba ee Bwana katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth. Jinsi ambavyo moyo wako ee Bwana  ulivyojaa upendo kwa ajili ya watu wako. unasema nasi  kwa njia ya ndoto hata kama hatujui  au kujali ee Bwana unatusemesha mara ya kwanza, unatusemesha mara ya pili, tatu unatusemsha ee Bwana lakini hatuna ufahamu ee Bwana  hatuelewi kuwa kuna ujumbe mkubwa umefichika ndani yake. Ee Mungu katika jina la Yesu  pamoja na viashiria  unavyoweka ndani labda tunavifuatilia kidogo  na kuviacha na mateso  yanatufuata ee Bwana  miaka na miaka  na roho zilizopita hapo ambazo sio nzuri  zinaambatana miaka na miaka na afadhali zingekuwa roho nzuri zikapita hapo. Maana kwa Yakobo ilikuwa ni roho nzuri  ambayo ilipita alipokuwa amelala  kule nyikani ameweka  jiwe kama mto akalala na akaota ndoto na akapata Roho Mtakatifu  ambaye alikuwa mahali pale  na akaenda nae na akaambatana nae  kila mahali alipoenda na Roho akajifunua kwake na kumwambia mimi ni Mungu wa Betheli  inawezekana Yakobo  alifikiri ni ndoto tu lakini kumbe Roho imeambatana pamoja na miaka 14 baadae  ikajifunua ee Mungu katika  jina la Yesu  watoto wako hawa  hawajajua / hatujajua ni kitu gani tumeokota katika hizi ndoto ee Mungu katika jina la Yesu.  Kumbe kuna maroho mabaya yanayo ambatana pamoja nasi  usiku na mchana yanayofuatana nasi na kuharibu maisha yetu, kuvuruga ndoa, biashara na uchumi na kuharibu maeneo mbali mbali na kuvuruga mahusiano  katika familia ee Mungu katika jina la Yesu.  Tumekuja mbele zako ee Bwana siku ya leo tunaomba  ufahamu juu ya ndoto . Tunajua ulimpa Daniel ufahamu juu ya ndoto  tunaomba utupe na sisi maana ulisema “kila aliye na kiu na aje kwangu”. kiu tuliyonayo ee Bwana ni kupata ufahamu juu ya ndoto  tuweze kuifahamu ee Bwana  Kibiblia  sawa sawa na maelekezo yako ee Bwana asinyanyuke mtu yoyote  akiwa na ujuzi wake  maana hata walipoitwa wenye hekima. Wachawi walienda Pia na wanganga lakini hawakuona kitu cha kumueleza Nebukadreza  hawakuona kitu cha kumsaidia Farao maana maelekezo yalikuwa yametoka kwako. Mungu  katika jina la Yesu mpe baba,mama, Kijana, Msichana, Mtoto  huyo ufahamu kwa ajili ya ndiyo. Mpaka kwenye Youtube, Ustream, CD,DVD, Kwenye Redio,  Facebool, Whatsapp,  na mahali popote wanapofuatilia semina bii ee Bwana katika jina la Yesu. Pokea ndani ya Fikra zako, nafsi yako, Roho yako na Mwili wako. Ufahamu wa ki-Mungu katika jina la Yesu Kristo ndani ya ndoto mbali mbali na uweze kuunganisha  kati ya ndoto na neno la Mungu katika jina la Yesu. Roho Mtakatifu Ambaye anatumia ndoto na neno la Mungu  na anazungumza na wewe katika jina la Yesu×3. Wakumbushe zile ndoto ee Bwana  ambazo zilikuwa na kitu  kiko ndani yake na hawajadaka, Mungu  rudisha ndani yao  kama vile unarewind ee Bwana  rudisha ndani yao. Kama ulivyomteremshia Yusufu wa Mariam   hukumpa tu ndoto bali ulimpa na ufahamu. maana alijua ya kwamba si tu kwamba ilikuwa ndoto bali  alijua kwamba umemtuma malaika wako  alijua ya kwamba ujumbe ule ni wa saa ile  alijua ya kwamba umekuja kubadilisha msimamo wake. Alijua ya kwamba neema yako imemtembelea ili umrehemu  ili miguu yake isije ikaingia  shimoni. ee Mungu katika jina la Yesu  tusamehe  ee Bwana Mahali ambapo  hatukutilia maanani. Tusamehe ee Bwana  tunapokuja mbele zako kutafuta ufahamu ya jinsi hii maana hatu kuutafuta mapema na tumejikuta  tumeingia kwenye mashimo. Ee Mungu tutoe kwenye hayo mashimo .. ee  tutoe katika vifungo na katika minyororo  tusaidie katika jina la Yesu.  Ameeen!!

Mpigie Bwana Yesu makofi…👏👏👏👏

Tuonane tena kipindi kijacho na Mungu akupe neema ya kuvuka na ombea semina hii ili Mungu atuvushe wengi na semina hizi ziwe msaada katika maisha yetu.

*……”Jesus Up”……*

✋✋✋✋✋✋✋✋✋✋

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA HIZI HAPA

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

ondoa jiwe iliujibiwe maombi yako