GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

JINA LA YESU NI UFUNGUO WA MAISHA YAKO

JINA LA YESU KRISTO – MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNIOctober 19, 2012 3:38 pm“Nami nakuambia ….. na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milangoya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:18 – 19).Maneno haya ya Yesu Kristo yanatuonyesha kuwa, nia yake ni kulijenga kanisa lililo na mamlaka kuliko shetani. Kanisa ni mwili wake (Waefeso 1:22 – 23). Wakristo waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo ni viungo vya mwili wa Kristo – ni viungo vya kanisa (1 Wakorintho 12:12, 13,27). Kwa hiyo Yesu Kristo anaposema atalijenga kanisa lake wala milango ya kuzimu haitalishinda – ana maana ya kuwa, kila mkristo aliye wake anajengwa kiroho awe na mamlaka ya kumshinda shetani.Ni budi tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufungue kama hakuna kitu cha kukifungua. Hawezi kutuambia tufunge kama hakuna kitu cha kufunga. Kwa hiyo ni lazima kuna vitu vya kuvifungana kuna vitu vya kuvifungua.Pia, tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezikutuambia tufunge na kufungua kabla hajatupa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo. Uwezo na mamlaka tunapata ndani ya Kristo aliyetukabidhi funguo za ufalme wa mbinguni.Itakuwa haina maana kwa Yesu Kristo kutukabidhi funguo bila ya kutufundisha namna ya kuzitumia. Hawezi kutukabidhi mamlaka bila kutufundisha namna ya kuyatumia.Yesu Kristo anasema tukifunga au tukifungua, mbinguni nako kunatia mhuri kitendo hicho. Hatuwezi kufanya hivyo kama tulichokifanya hakifanani na mapenzi yake. Ndiyo maana tunaomba kuwa mapenzi yake yatimizwe hapa duniani, kama yanavyotimizwa huko mbinguni. Kwa maneno mengine tunawezakusema ya kuwa ukifanya kitu chochote katika mapenzi ya Mungu, Ufalme wa mbinguni utakuwa upande wako.Aina za Funguo:Biblia inazungumza juu ya funguo za aina tano zifuatazo:Funguo za Ufalme wa Mbinguni – Mathayo 16:19 – Yesu Kristo amekabidhi funguo hizi kwa wakristo (Kanisa).Funguo za mauti na za kuzimu – Ufunuo 1:18 – Funguo hizi anazo Yesu Kristo – baadaye atampa Malaika mmoja funguo za kuzimu ili amfunge Ibilisi (Ufunuo 20:1-3).Ufunguo wa nyumba ya Daudi – Isaya 22:22; Ufunuo 3:7. Ufunguo huu anao YesuKristo.Ufunguo wa kawaida wa mlango – Waamuzi 3:25.Neno ‘funguo’ lililoandikwa katika Mathayo16:19; Ufunuo 1:18; Isaya 22:22 na Ufunuo3 – 7 lina maana ya ‘mamlaka’. Kazi ya funguo ni kufunga na kufungua. Kwa hiyo ukipewa funguo maana yake umepewa mmalaka ya kufunga na kufungua.Kwa mfano, mtu akikupa funguo za chumba – maana yake una mamlaka juu ya chumba hicho kukifunga na kukifungua.Mtu yeyote akitaka kuingia kwenye chumba hicho hawezi kufanya hivyo bila kupata ruhusa toka kwako ya kumfungulia.Ukipewa funguo za gari maana yake kwa muda huo ambao una funguo hizo za gari, una ‘mamlaka’ juu ya hilo gari kulifunga lisitumike au kulifungua litumike. Mtu akitaka kulitumia ni budi aje kwako kwa ajili ya kufuata funguo.Kwa hiyo Yesu Kristo aliposema ametupa funguo za ufalme wa mbinguni alikuwa ana maana ya kuwa ametupa ‘mamlaka’ ya ufalme wa mbinguni. Ni vizuri ufahamu hapa ya kuwa ufalme wa mbinguni ni ufalme wa Mungu ulio na mamlaka juu ya falme nyingine zote – ufalme wa shetani, ufalme wa wanyama, ufalme wa wadudu, ufalme wa mimea, ufalme wa ndege, na kadhalika. Ikiwa wewe ni mkristo uliyeokoka basi fahamu ya kuwa, una mamlaka uliyopewa na Yesu Kristo juu ya falme hizi zote!Yesu Kristo anaendelea kusema kuwa; lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.Kwa mfano ukiamua kumfunga ibilisi asikusumbue katika maisha yako, mbinguni pia wanasimamia utekelezaje wajambo hili. Hata kama ibilisi ataamua ‘kukata rufaa’ juu ya uamuzi wa kumzuia asikusumbue na akaenda kwa Mungu kuomba aachiliwe – Mungu atamwambia ‘rudi kwa aliyekufunga, akikufungua nami nitakufungua, lakini asipokufungua nami sikufungui’Unaweza kusema mbona shetani alipewa ruhusa na Mungu kumjaribu Ayubu. Kumbuka kuwa Ayubu aliishi katika agano la kale na sisi tunaishi katika agano jipya ambalo ndani yake tuna mamlaka ya kumfunga shetani kwa jina la Yesu Kristo.Kuna wakristo wengi wameonewa na ibilisikwa kuwa hawajui mamlaka waliyo nayo na namna ya kuyatumia.Jambo jingine ninalotaka uone hapa ni kwamba Yesu Kristo alisema ametupa “funguo ZA ufalme wa mbinguni”; na hakusema ametupa ufunguo wa ufalme wambinguni.Neno hili ‘ZA’ lina maana ya kuwa kuna funguo za ufalme wa mbinguni zaidi ya mmoja. Kumbuka kuwa kuna tofauti ya funguo za ufalme wa mbinguni na zile funguo za mauti na za kuzimuFunguo za mauti na za kuzimu alikuwa nazo shetani hadi aliponyang’anywa funguo hizo na Yesu Kristo kwa kufa kwake msalabani na kufufuka. Funguo za mauti na za kuzimu anazo Yesu Kristo sasa.Funguo za ufalme wa mbinguni anazo Yesu Kristo, lakini amezikabidhi kwa wakristo waliomo duniani wazitumie.Ukifuatilia maneno yaliyomo katika agano jipya utaona ya kuwa kuna funguo NNE za ufalme wa mbinguni nazo ni:1. Jina la Yesu Kristo2. Damu ya Yesu Kristo3. Neno la Yesu Kristo4. Nguvu za Roho MtakatifuKatika somo hili tunajifunza juu ya jina la Yesu Kristo ambalo ni mojawapo ya funguo za ufalme wa mbinguni.Tumia mamlaka uliyopewa:Kuna wakati fulani ambapo nilihangaika siku nyingi kwa kuomba na kwa kulia usikuna mchana ili shida niliyokuwa nayo iniondoke bila mafanikio. Nilikuwa naombakwa Mungu, lakini sikuona mabadiliko yoyote, ilikuwa kama vile Mungu ameziba masikio yake asisikie maombi yangu. Pamoja na maombi niliongeza kulia zaidi lakini sikufanikiwa pia.Nikiwa katika hali ya kukata tamaa huku nikijiuliza kwa nini naomba kwa Mungu lakini shida inayonisumbua haiondoki – Roho Mtakatifu alisema ndani ya roho yangu maneno haya; “shida yako inayokusumbua imeletwa na shetani. Unayo mamlaka ya kumkemea shetani naye ataondoka na shida uliyonayo itakwisha. Kama hufahamu juu ya mamlaka uliyonayo soma vitabu vya Waefeso, Wafilipi, Wakolosai na vitabu vingine katika Biblia”Niliposikia maneno hayo nikaomba tena; “Ee Bwana nifundishe juu ya mamlaka uliyonipa ili nipate kuyatumia.”Namshukuru Mungu ya kuwa alisikia sala yangu na alianza kunifundisha juu ya mamlaka aliyonipa, na bado anaendelea kunifundisha hatua kwa hatua kila siku.Nilipoendelea kujifunza ndipo nilipotambuakuwa si kila shida uliyonayo itaondoka kwamaombi – bali shida nyingine zinaondoka kwa KUAMURU katika jina la Yesu Kristo shida hiyo iondoke au kwa KUAMURU hali unayoitaka itokee.Kwa hiyo siku moja usiku niliamua kutumia mamlaka niliyonayo katika jina la Yesu Kristo shetani aondoke katika eneo alilokuwa ananiletea shida – mara hiyo hiyo kulitokea mabadiliko. Shida iliyonisumbua kwa muda mrefu ilitoweka mara moja. Badala ya kusubiri Mungu afanye kitu kwanza juu ya shida hiyo, niliamuru iondoke na Mungu akasimamia utekelezaji wake!Ndivyo alivyomaanisha aliposema “Lolote utakalolifunga (wewe!) duniani, litakuwa limefungwa mbinguni” – Maana yake Mungu atausimamia uamuzi wako wa kulifunga hili jambo! Ukiamua kulifunga, Mungu atalifunga pia! Anayeanza kufanya kitu ni wewe!Hivi ndivyo Mtume Petro alivyofanya alipomkuta yule mtu aliyekuwa kiwete tangu tumboni mwa mama yake – wakati huo alikuwa ana umri usiopungua miaka arobaini akiomba sadaka katika mlango wa kuingia hekaluni.Mtume Petro alipomwona hakumwomba Mungu amponye bali alimwamuru asimame na kutembea kwa Jina la Yesu Kristo! Alisema hivi; “Kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende”. Halafu; “Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. (Yule aliyekuwa kilema) Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda, akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akirukaruka, na kumsifu Mungu” (Matendo ya Mitume 3:6 – 8).Kile alichoamuru Mtume Petro kitokee kwa jina la Yesu Kristo kilitokea. Alimwamuru yule kilema asimame na kutembea kwa jina la Yesu Kristo na ikawa hivyo!Na wewe unaweza kufanya hivyo ikatokea! Kwa nini? Kwa sababu na wewe umepewa jina la Yesu Kristo lenye uwezo usiobadilika! Kumbuka Yesu Kristo alisemahivi;“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya” (Marko 16:17-18).Labda umeyasoma maneno haya mara nyingi kiasi kwamba umeyazoea, na yameanza kupoteza uzito wake. Ni maombi yangu kwa Mungu kuwa Roho Mtakatifu ayahuishe upya maneno haya ndani yako ili uyaone kama Yeye anavyotaka uyaone.Siku moja nilikuwa nafundisha neno la Mungu mahali fulani, na baada ya mafundisho alijitokeza mtu mmoja aliyesema anaumwa kifua na kwamba aliihitaji aombewe.Nilimwambia aweke mkono wake kifuani mahali alipokuwa anaumwa – na akafanya hivyo. Na mimi nikaweka mkono wangu juu ya mkono wake uliokuwa kifuani pake, halafu nikasema “Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti”! Nilipotamka tu jina hili la ajabu, yule mtu akaanguka chini na majini yaliyokuwa yanabana kifua chake na kuleta maumivu yalianza kupiga kelele. Nikayaamuru yamtoke mtu huyo kwa jina la Yesu Kristo – na yakamtoka wakati huo huo – mtu huyo akasimama akiwa mzima!Kwa nini ilikuwa hivyo? Kwa kuwa Yesu Kristo alisema kwa jina lake tutatoa pepo! Na ndivyo ilivyo! Tumia mamlaka uliyo nayo usiogope! Ikiwa wewe ni mwamini yaani umeokoka, jina la Yesu Kristo ni lako – ni uamuzi wako kulitumia au kutokulitumia.Siku nyingine niliitwa kwenda kumwombeamama mmoja ambaye alikuwa hawezi kuinuka kitandani kwa muda wa miezi miwili kwa sababu ya ugonjwa wa homa. Nilipofika katika nyumba hiyo niliweka mkono wangu juu ya kichwa cha mama yule na kuiamuru homa imwache kwa jina la Yesu Kristo, kisha nikaondoka. Nilimwacha yule mama akiwa amelala. Kesho yake mtoto alikuja kuniambia kuwa mama yake amepona, ameamka toka kitandani na anafanya kazi! Jina la Yesu Kristo libarikiwe milele.Yesu Kristo alisema tukiweka mikono yetu juu ya wagonjwa kwa jina lake, watapata afya. Na ndivyo inavyotokea tukitii agizo hili. Kuna uweza usiopimika katika jina la Yesu Kristo. Ni ufunguo unaowafungua watu toka katika minyororo ya shetani. Usiogope. Uwe na moyo wa ushujaa na ujasiri mwingi – tumia mamlaka uliyonayokatika jina la Yesu Kristo.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA HIZI HAPA

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

ondoa jiwe iliujibiwe maombi yako