GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

KUFUNGA NA IMANI

Kufunga na Imani Mara nyingi katika Biblia maombi ya watumishi wa Mungu yaliambatana na kufunga; 1. Walifunga wakati wa hatari (Esta 4:3), 2.Wakati wa masikitiko (Nehemia 1:3-4), 3.Wakati wa kutafuta mwongozo wa Mungu (Daniel 9:1-3), 4. Wakati wa kutubu (Yoeli 2:11-12), 5. Wakati wa kumwabudu Mungu (Matendo 13:1-2), 6. Wakati wa kuweka wakfu viongozi (Matendo 14:23), 7 Pia Yesu alifunga kabla hajaanza huduma(Mathayo 4:1-2). Kufunga kunahitajika wakati tunataka kuona mabadiliko makubwa ya kanisa na sisi binafsi, soma Yoeli 2:12-13. Kufunga kunatuwezesha kujinyenyekeza kwa Mungu na kutukumbusha kwamba sisi ni dhaifu tunahitaji msaada wake. Kunatuwezesha kuwa na muda mrefu wa kuomba na kuacha kufikiria chakula na mambo mengine ambayo yanaweza kutufanya tusimaanishe katika kuomba. Kufunga kunatuwezesha kuwa na nidhamu ya kula na kuuzuia mwili katika tamaa, kama ya uzinzi, hasira, uchoyo nk. Ukifunga mara kwa mara ni rahisi kuwa mtoaji (Isaya 58:6-7). Kufunga ni ishara ya nje inayoonyesha tuko tayari kuyatoa maisha yetu mbele za Mungu, maana chakula hutuwezesha kuishi, hivyo kutokula ni ishara ya kuutoa uhai wetu. Ukiombea mtu kwa kufunga ni kama vile umetoa sehemu ya uhai wako kwake. Biblia kuhusu Yesu inasema, “Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.” (Mathayo 4:2). Watu wengi wanaamini kwamba neno hili linalo onyesha kwamba Yesu alifunga siku arobaini kisha akaona njaa, badala ya kiu, lina ashiria kwamba Yesu alikunywa maji. Sababu ni kwamba mtu asipokula muda mrefu kitu cha kwanza anachotamani ni maji sio chakula. Kunywa maji wakati wa kufunga si udhaifu, ni hekima. Kwa hiyo ni vema ukifunga muda mrefu unywe maji kwaajili ya afya yako na kulinda heshima ya jina la Yesu lisitukanwe kwa kutokujua kwako. Unaweza kutokunywa maji masaa 12, 24, 48 au 72. Baada ya hapo inashauriwa unywe maji. Hata hivyo kwa ujumla ni vizuri unywe maji wakati wote unapofunga. Kama husikii kunywa maji baada ya siku tatu ni vizuri uwe na uhakika Mungu amekuongoza kufanya hivyo. Kufunga na kuomba ni kichocheo cha imani zetu, ili ziweze kutenda na kusema yasiyowezekana. Yesu alisema, “Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana , amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] (Mathayo 17:20-21). Kwa kifupi katika andiko hili Yesu alisema kuna namna ya matatizo ambayo hayawezi kutoka mpaka imani zetu zichangamane na kufunga na kuomba. Kufunga kunaweza kufungulia nguvu ya Mungu katika maisha yetu na kanisa kwa namna ambayo isingewezekana kwa jinsi nyingine. Sababu ni kwamba nguvu za Mungu huonekana katika udhaifu. Ukiwa na nguvu kama wewe huna haja ya nguvu ya Mungu, ukiwa huna nguvu na kumwita Mungu kwa kufunga katika udhaifu huo wa mwili wako Mungu ataonekana. Maana neema ya Mungu hujidhihirisha katika udhaifu au kutoweza (2Wakorintho 12:9). Kufunga ni ishara ya nje inayomwambia Mungu, “mimi ni dhaifu siwezi nakuhitaji kwa imani”.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA HIZI HAPA

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

ondoa jiwe iliujibiwe maombi yako