GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

KUFUNGULIWA KUTOKA KWENYE MIZIMU,MASHETANI,MAPEPONA.VINYAMKELA PIA NA LAANA ZA UKOO

KUFUNGULIWA KUTOKA ROHO ZA MIZIMUMizimu (family spirit) ni mapepo yaliyotokana na malaika walioasi pamoja na shetani ambayo watu waliyafanya kama ndugu kutoka kizazi hadi kizazi.Mizimu no roho za shetani ambazo ni chukizo kwa MUNGUKumbukumbu 18:9-12 ''Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, MUNGU wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale.Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, MUNGU wako, anawafukuza mbele yako.''yanayozungumza hapo tuliposoma ni kuwahusu WAGANGA WA KIENYEJI, WACHAWI, WANAJIMU,WASIHIRI NA WANAOWAOMBA WAFU, mambo ambayo yote ni machukizo kwa MUNGU na wote hawa wanatumia mizimu kufanikisha mambo yao na kwa wale wanaomba maiti(wafu) hawa wanaomba mizimu hivyo wanahusika moja kwa moja na mizimu maana mtu aliyekufa hawezi kamwe kukusikia na hata kama anakutokea usiku tambua tu kwamba ni mizimuambayo ni majini yanavaa sura ya ndugu yako na kuja kwako na kumbuka kuwa jini anaweza kuiga kila kitu kuanzia sauti hadi sura na kwa sababu shetani anataka umkosee MUNGU wako kwa kumtii yeye, atakuambia mambo mengi ya kufanya, Yupo mama mmoja alikua anatokewa na mama yake nakumwambia kwamba''siku hizi umenisahau kabisa hata kaburi langu hufagii hivyo kesho asubuhi sana kafagie na unyunyuzie damu ya kuku juu ya kaburi langu.jambo hilo lilipelekee yule mama kwenda kwa mganga wa kienyeji nakumbuka kuwa hakuna mganga wa kienyeji asiyetumia mizimu.akajikuta anahusika na mabomabaya zaidi hadi kumua mtoto wake maana yule mzimu alianza kwa kutaka damu ya kuku baadae anataka kafara ya damu ya mtoto wa yule mama maana ilifika kipindi vitisho vikawa vyingi na kwa sababu mama yule alishaingia maagano na mizimu ile kwa kutii maelekezo ya kwanza akaanza kupata shinda sana na akaambiwa atapata mikosi maisha yake yote na hali hiyo ikapelekee kuua mtoto wake na cha ajabu shetani alimtumia yule mganga wa kienyeji kuongeza vitisho kwa mama na kutoa ushauri wa kumwua mtoto. Ndugu zangu jina la YESU KRISTO pekee linaloweza kuondoa mizimu maishani mwako hivyo kama unasumbuliwa na mikosi ya ukoo, mizimu ya ukoo, utasa au magonjwa ya ukoo basi kimbilia kwenye maombezi katika kanisa la kiroho karibu na wewe na utafunguliwa na kuwa salama kabisa mbali nalaana zote za ukoo na mashariti ya kishetani. na katika BIBLIA kitambu chaMambo ya walawi 19:4 inasema ''Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi BWANA, MUNGU wenu.'' ndugu moja ya miungu ambayo wanadamu wanaiabudu ni mizimu na kumbuka kwamba waganga wa kienyeji wanatumia mizimu katika kazi zao na ndio maana mama mmoja ambaye sasa ameokoka alikua mganga wa kienyeji zamani aliwahi kuniambia kuwa kama mgojwa mwenye majini akija kwake kutibiwa yeye anachofanya anaongeza majini ndani ya mgojwa na kumpa mashariti ya kufanya ili abaki mzima na moja ya mashariti hayo alikua anawaambia wateja kurudi kwake kila baada ya miezi mitatu maana anajua muda wa majini kutaka ndamu umefika na kila mteja akija lazima aje na kuku mwenye rangi moja kama ni mweupe awe mweupe pote na kama ni mweusi awe mweusi pote.Katika 1 Samweli 28:7 BIBLAI inasema''Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuulizakwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.''Huyu Sauli alikua ni mfalme wa taifa la Israel ambaye aliamua kuwafuata waganga wa kienyeji na kitendo hicho kilikua ni machukizo makuu kwa MUNGU na kupelekea kunyang'anywa ufalme akapewa Daudi na huyo sauli akafa vitani na jambo lile wa kwenda kwa waganga liliongeza balaa kwa taifa badala ya kupunguza . Nduguplease please usikubali kwenda kwa waganga wa kienyeji wala usoma nyota maana watakupoteza na utakua mbali sana na MUNGU wako aliyekuumba na hakika kwa kitendo hivyo utakua unajichimbia shimo mwenyewe. ni hrei kumpelekea BWANA YESU shida zako na yeye ni mwaminifu na wa haki atakuponya na utakua huru daima maana amesema katika Mathayo 11:28 kwamba ''Njoni kwangu, ninyinyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha''MUNGU akubariki sana wewe usiye na mizimu maishani mwako maana ulimpa BWANA YESU maishayako na ukatengwa mbali na mizimu ya ukoo ambao ipo katika kila mtu ambaye hajasafishwa kwa damu ya YESU maana mizimu hiyo ipo tangu kizazi na kizazi na mambo mengi yanawapata ukoo fulani fulani tu kwa sababu ya mizimu, ukielewa hivyo chukua hatua kwa kumpa YESU maisha yako na utakua huru pia utakua ufunguo katika ukoo wetu kuwafukuza mizimu ya mababu ambayo imeleta balaa kubwa katika maisha. maana wapo watu wao wanajifahamu ni watu wasio na akili shuleni yaani ukoo mzima hakuna anayeweza kufauli kwenda sekondari na hawajui tatizo ni nini lakini kumbe tatizo ni mizimu ya ukoo.mungu akubariki sana endelea kutembelea uta pata habari za injili..

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA HIZI HAPA

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

ondoa jiwe iliujibiwe maombi yako