GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

MADHABAHU. ZA KICHAWI ..KISHETANI~NA ZA KIPEPO ZA VUNJWA KWA DAMU YA YESU

SOMO: MADHABAHU YA KUSHINDWA Madhabahu ni eneo linalojengwa na mtu au watu kwa ajili ya kutolea kafara. Kafara hii yaweza kuwa mbuzi, ng’ombe au mwanadamu. Ziko madhabahu maeneo mbalimbali zilizojengwa ili kila jambo atakalolifanya mtu fulani lisifanikiwe. Mtu anaweza kufungua duka halafu baada ya muda akalifunga kwasababu ya kutokufanikiwa kinyume na matarajio yake. Kila analolifanya linashindikana, anakuwa mtu wa kushidwa shindwa. Mtu wa aina hii anatakiwa kutambua kuwa kuna madhabahu ya kushindwa aliyotengenezewa. Madhabahu inaweza kuwaleta watu pamoja, kumwabudu na kusema na Mungu wa mbinguni au shetani. Unaweza kufika madhabahuni pa BWANA ukiwa mgonjwa lakini ukaondoka mahali hapo ukiwa mzima. Na hii ni kwa kuwa, madhabahu ni daraja la kumkutanisha Mungu na mwanadamu. WATU WALIOMJENGEA MUNGU MADHABAHU KATIKA BIBLIA IBRAHIMU Ibrahimu, baba wa imani aliambiwa na Mungu atoke katika nchi aliyozaliwa ya uru wa wakaldayo na aende katika nchi ya mbali BWANA atakayomuonyesha, na amjengee BWANA madhabahu huko. Ibrahimu alitii neno la BWANA na akamjengea madhabahu. Imeandikwa; Mchungaji Mwandamizi Baraka Thomas Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. 8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Mwanzo 12:7-8 Kupitia madhabahu hii aliyoagizwa kujenga Ibrahimu aliweza kuwasiliana na Mungu. Imeandikwa; Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. Mwanzo 22:9 Ibrahimu alikuwa mtu aliyefanikiwa sana kutokana na madhabahu aliyoijenga. Kumbe madhabahu ni kiunganishi cha Baraka kutoka kwa Mungu anayeabudiwa kwenye madhabahu husika mpaka kwa anayeabudu. Hivyo ni dhahiri kuwa mikosi, balaa na matatizo mengine pia yana chanzo chake kutokea kwenye madhabahu. Kwa akili yako unaweza kuhisi kuwa kushindwa kwako ni kwasababu ya elimu yako ulionayo, au mtaji kidogo ulionao. Mawazo yako sio kweli wala sio sahihi, tambua kuwa kuna madhabahu imejengwa inayofanya kazi ya kupolomosha mambo yako. Leo kwa jina la Yesu tunabomoa kila madhabahu ya kushindwa kwako. Katia nyakati tulizonazo leo, watu wanamjengea shetani madhabahu kwenye magari yao, ofisi zao na hata nyumba zao. Kutokana na madhabahu hizi, waweza kuona mtu anapandishwa cheo bila kustahili; wakati yule aliyestahili anahamishwa ofisi ghafla au anakufa. Ni madhabahu ya kushindwa imefanya kazi. Mwimbaji John Lisu Bwana akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu. Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko. Mwanzo26:24-25. Utaona Isaka kama ilivyokuwa kwa baba yake, yeye pia anamjengea MUNGU Yehovah madhabahu. Ili uweze kuwa na uhusiano wa kudumu Mungu uweze lazima umjengee madhabahu. Pia tunaona kuwa anachokifanya baba mara nyingi mtoto naye hukifanya; hivyo aliyeabudiwa na baba mara nyingi ndiye ambaye huabudiwa na mwana. Madhabahu inaweza kuwa chanzo cha Baraka zako au shida yako. Hivyo madhabahu zilizojengwa na wazazi wako au watu wa kale katika ukoo wako yaweza kuwa ndio chanzo cha Baraka au kushindwa kwako leo. Mfano Gideoni, alikuwa amekuwa mtu dhaifu kwa sababu alikuwa ameteswa na madhabahu ya kishetani iliyokuwa imejengwa na baba yake. Kila madhabahu inayojengwa hujengwa kwa sababu maalum. Ipo madhabahu imejengwa mahali kwa jina lako ili ushindwe na kufa katika matatizo uliyonayo. Unyonge wako ni kwasababu ya madhabahu iliyojengwa ili ikutese. Leo tutawaagiza malaika wa BWANA wazisake madhabahu za kushindwa zilizokufunga kwa muda mrefu sana. UKIRI: MIMI NI SHUJAA WA BWANA, KWA MSAADA WA BWANA NALIENDEA JESHI NA KULIKANYAGA. NALIPONDA NA KULIONDOSHA KWA JINA LA YESU. NUHU Nuhu mara baada ya kutoka kwenye safina alimjengea BWANA madhabahu na kuweka sadaka mbele zake. Unapotaka kumtolea Mungu unapashwa kumtolea kilichosafi. Ili madhabahu iwe na nguvu lazima kuwepo sadaka juu yake tena iliyosafi. Mfano Habili alimtolea Mungu sadaka nono na yakupendeza na Mungu akapendezwa nayo. Ni vizuri kujiuliza kwanza kabla ya kumtolea Mungu sadaka kuwa unatoa nini mbele za BWANA? Mara baada ya sadaka ya Nuhu mbele za BWANA, Mungu akafanya agano na Nuhu kuwa hataiangamiza tena nchi kwa gharika kama lile, na akaweka ishara ya upinde wa mvua. Imeandikwa: Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.Mwanzo 8:20 Unaweza kutafuta kwa taabu sana, hali ikawa nzuri baada ya taabu kubwa lakini kama kuna madhabahu ya kushindwa imejengwa kwa ajili yako utaishia kufa mara tu baada ya kupata. Tambua kuwa unapaswa kupigana na kushindana ndio amani ya maisha yako iweze kupatikana. Usisubiri kufarijiwa, faraja unatakiwa kuitafuta wewe mwenyewe kwa kupigana na kushindana juu ya ufalme wa giza. Imeandikwa: Kwa maana kushindana kwetu sio juu ya damu na nyama…. Waefeso6:12

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

SOMO: MWONGOZO WA KIBIBLIA WA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO