MAOMBI YA KULIA .,KUOMBOLEZA .NA KUFUNGA KWA MZIGO
MAOMBI YA KUFUNGA, KULIA, NA KUOMBOLEZA. Isaya 30:49-21Ni maombi yeye mzigo moyoni mwa mtu, ni maombi yenye utungu. (Yoe.16:20-24)Kulia mbele za Mungu – Lu. 23:38, Ebr. 5:7-10; Ebr. 5:7-10, Yer.31:9KUFUNGA - Yoel. 2:12-A. MAANA KWA MTIZAMO WA AGANO LA KALE KUHUSU KUFUNGA• Kwa mtizamo wa agano la kale ni kujinyima chakula na vinywaji ili kumwomba Mungu au kufanya kitu kwa ajili yake.• Ilikuwa ni ahadi yenye kiapo, kwamba mtu asipofanya hivyo kwa uaminifu, inakuwa kwake ni dhambi, laana,na anastahili kupata mapigo au kifo cha papo kwa papo.• Ilikuwa ni kujitesa nafsi mbele za Mungu – Toba.• Ilikuwa ni kujinyima ili kumfanyia Mungu ibada au kazi.• Ilikuwa ni matokeo ya kushughulikia:-dhambi – ili kuleta upatanisho au tobamagonjwa – tauni, vita na misiba kuhitaji kuisikia sauti ya Mungu kwa ushauri na uongozi, kujiwekawakfu au nadhiri / kujitenga kwa ajili ya Mungu, ilikuwa ni adhabu kwa nafsi ya mtu au roho yake• mtu asiyefunga au aliyefanya kazi siku hiyo,watu walitakiwa kumpiga kwa mawe mpaka afe.Alipata mapigo toka kwa Mungu, alipata laana piakufunga ilikuwa ni kwa Lazima! Kwani ilikuwa ni KIAPO au NADHIRI mbele za Mungu.Kufunga kwa pamoja – ilikuwa mmoja akishindwa wengi wanaathirika au wanaadhibiwa – ganzi ya meno?Kulikuwa ni kufunga kwa namna ya kidini, mtu alifanya kwa kutii tararatibu au mapokeo ya kidini tu. (Zekaria 7:4-14; -BWANA HAKUWEPO SAYUNI - HAWAKUWA NA MUNGU KATIKA KUFUNGA KWAO.Waling’ang’aniakufunga bila uelekevu wa moyoWalikosa hukumu ya kweli, rehema, na huruma.Walifunga lakini bado walikuwa wanawaza mabaya mioyoni mwao – Kama fisi aliyekuwa akiungama dhambi yakuua mbuzi mbele ya padri katika kitubio halafu mara akamuona mbuzi anapita nje, akamwambiapadri,tafadhari padri, niungamishe haraka, mbuzi anapita nje, asije akapotelea mbali, nataka nikamuwahi.Ilikuwa ni huduma ya mauti, huduma ya adhabu, japo ilikuja katika utukufu – huduma ya andiko si ya roho. 2Kor. 3:7-11B. KUFUNGA KWA MAANA YA KIROHOSwali: Zekaria. 7:1-8:23; Je, yanipasa kufunga?• Jibu: Kula ni kwa ajili ya nafsi zao – ziishi wasife.• Kufunga pia ni kwa ajili ya nafsi zao – zipate kuwa hai kiroho!• Ni muhimu kula na kuishi (mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu – lazima litunzwe) – mazoezi ya kimwiliambayo yafaa.• Ni muhimu zaidi kufunga pia ili kuishi na kuwa hai kiroho mbele za Mungu – ni mazoezi ya utauwaambayo yafaa zaidi.Ni kufunga kwa ajili ya kuyaonea wivu mkuu mambo ya Mungu – yafanikiwe!Ni kuwa na kiu kwamba utukufu wote apewe BWANA YESU, lakini ibilisi aaibishwe!Ni kufunga ambako UPO NA BWANA PAMOJA NAWE, UPO NA BWANA ARUSI• hivyo kufunga kunakuwa ni Furaha na Shangwe– Sherehe!• kunakuwa si huzuni, mzigo, wala kwa kuona kuwa ni mateso, japo unaweza kuteseka.• huwa ni kufunga ambako si kwa lazima, bali ni kwa hiari ya moyo na kwa kujitoa kwa furaha.• si kwa kujionyesha kwa watu au kujitangaza au si kwa kutaka sifa kwa watu.• sio kwa kujitakia haki yako mwenyewe mbele za Mungu, (Rum. 10:1-4)• ni kufunga kwa kadiri ulivyojaliwa na Mungu – yaani iwe kufunga kwa kawaida au si kwa kawaida,inategemea unavyoongozwa na Mungu.• Si kwa kumwangalia au kujilinganisha na mtu mwingine• ni kufunga kama vile ulivyokusudia moyoni mwako / ulivyopanga – bila kigeugeu.• huwa ni kujitoa kwa bidii, maana utapewa taji naBWANA.• Ni kufunga kwa imani.• Ni huduma yenye utukufu zaidi – huduma ya roho si ya andiko.SABABU ZA MAOMBI YA KUFUNGA• Ni tabia ya wana wa Mungu kufunga tangu – Sethi (Mwa. 4:26)• BWANA YESU alifunga pia – aliye mzaliwa wa kwanza wa wana wa Mungu.• Ili kuutafuta uso au uwepo wa Mungu na kumkaribia Mungu na kumpinga shetani.• Ili kumheshimu Mungu wetu kwa• kumfanyia ibada – Mdo 13:1-3• kujinyenyekeshambele zake kwa kuutiisha mwili• kuonesha TOBA mbele za Mungu – kujitesa, kuiadhibu roho. Zab.69:10.• Kuutafuta muda mzuri zaidi wa kuomba• kuutoa uhai wetu kwa MunguIli tupate nguvu za kiroho (kama tunavyopata katika kusifu, kuabudu, na kusoma neno la Mungu• ni aina ya funguo kwa yale yasiyowezekana kwanamna ya kawaida (Esta kwenda mbele za mfalmekinyume na kawaida)• ni nguvu katika kuifanya kazi ya Mungu (Mt.4:1)• Ili kuongeza nguvu ya imani yetu mbele za Mungu• ni kuongeza nguvu katika kuisikia sauti ya Mungu (kuituni sauti ya Mungu)• Nguvu katika kulindwa na Mungu• Kufunga ni silaha ya kiroho dhidi ya hila za shetani na majeshi yake.Ili kuifanya kazi ya Mungu• Kumfunga shetani, kuzitharibu kazi zake, na kuyafungua yote aliyoyafunga.• kujitoa uhai wetu kwa ajili yaw engine (1Yoh. 3:16)• ili kumtolea Mungu nafsi zetu kuwa dhabihu (Rum 12:1)Ili kumtii Mungu na kumpinga shetani.• Ni agizo la Mungu kwa neno lake.Kufunga ni muhimu sana!• Hata shetani na wajumbe wake hufunga! (Soma1Fal.21:1-29; Mdo.23:12-22) Hufunga ili kuongezanguvu za kipepo.AINA ZA / NJIA ZA KUFUNGA – Isaya 58:1-14A. KUFUGA KWA KUACHA MAOVU YOTE – Mstariwa 6.• Kuacha kuwaza, kusema, kufurahia, kukubaliana nayo, kushirikiana nayo, kushirikishwa, kudhamiria/ kukusudia, au kutamani maovu. (Ebr.13:6)• Kupenda hukumu ya kweli, rehema, na amani.B. KUFUNGA KWA KUWA MTOAJI – Mstari wa 7.• Malimbuko, zaka, dhabihu (Sadaka ya hiari /matoleo),changizo, misaada, nadhiri, sifa, shukuraniC. KUFUNGA KWA KUACHA KULA – kumegawanyika aina kuu mbili, nazo ni:-i. KUFUNGA KWA KAWAIDA• Ni kufunga kwa chini au zaidi ya masaa 12• KUACHA VYAKULA, AINA FULANI, AU KUPUNGUZA KULAMfano; Daniel – alikula mtamaYohana mbatizaji – alikula asali na nzigeEliya – alilishwa mkate na maji kando ya kijito………………• KUACHA CHAKULA ILA KUNYWA MAJI TU – Mt.4:1-4; Kumb.9:9; Kutoka 34:28• KUACHA KULA CHAKULA NA KUTOKUNYWA MAJI – Bila kula wala kunywa iwe siku si zaidi ya tatu.ii. KUFUNGA KUSIKO KWA KAWAIDA• Ni kufunga zaidi ya siku tatu.• Ni kufunga ambako nguvu za Mungu zinaingilia kati na kumuwezesha mtu.Mfano: Eliya pia – 1Fal. 19:2-9; alilishwa kwanza chakula (alipewa nguvu) na malaika• Unakuwa unazo nguvu, hudhoofiki, wala hufi.• Hujisikii njaa wala kiu, hadi unapomaliza kufunga – Mt. 4.• Inawezekana kukawa ni kufunga chakula na wakati unatumia maji ya kunywa-absolutefasting.• Au kufunga wakati hautumii hata maji ya kunywa. – total fasting.1. Musa amewahi kufunga si chini ya mara mbili (Kumb.9:9,18; Kut.34:28 – hakula wala kunywa2. BWANA Yesu – alifunga kula; biblia haitaji kwamba hakunywa maji. Luk. 4; Mt.4:
Comments