GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

JINSI YA KUVUMILIA UKIKUTANA NA MAGUMU. SHIDA. MAJARIBU.

Baada ya mtu kuokolewa na anaendelea na wokovu, inampasa awe mvumilivu mpaka mwisho. Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani hakutenda dhambi kabisa katika maisha yake yote maana maisha yake yote yalikuwa ya uvumilivu.Ndivyo nasi tunapaswa tuwe wavumilivu (Gal. 5:22). Wana wa Israel walikosa uvumilivu wakamkosea Mungu na hayo yaliandikwa kutuonya sisi (1Kor 10:10-11, Warumi 15:4).Somo hili limegawanyika katika vipengele 6:1. MUNGU CHANZOCHA UVUMILIVU2. JINSI MUNGU ALIVYO MVUMILIVU3. UVUMILIVU SEHEMU YA IMANI YA MKRISTO4. HASARA YA KUKOSA UVUMILIVU5. FAIDA YA KUWA MVUMILIVU6. JINSI YA KUWA MVUMILIVU1. MUNGU CHANZO CHA UVUMILIVUMungu ndiye chanzo cha uvumilivu, maana Mungu kama asingekuwa na uvumilivu angeweza kuuteketeza ulimwengu huu wa wasiomcha Mungu. Mungu ametuvumilia hata sisi tulipokuwa wenye dhambi na hata tunapoanguka tenadhambini hajatuacha tufe kabla hatujaokoka ametuvumilia hadi tumeokolewa. Ndiyo nasi tunapaswa kuwa na uvumilivu tena kwa kuwezeshwa nay eye maana yeye ndiye chanzo cha uvumilivu2. JINSI MUNGU ALIVYO MVUMILIVUMungu hapendi watu watende dhambi lakini anaona wanadamu wanatenda dhambi lakini anavumilia tu ili waifikilie toba maana yeye hapendi mtu apotee (2Pet 3:9, Rum 2:4).Ukiyakumbuka mengi uliyoyafanya nyuma mabaya ya kila namna lakini Mungu amekuvumiliampaka leo upo hapa. Mungu aliwavumilia wana wa Israel miaka arobaini (40) walipokuwa njiani wakielekea Kanaani (Matendo 13:18-19). Mungu ni mvumilivu mno, kwa kila aliyeokolewa . siri kubwa ya kufanikiwa ni kuwa mvumilivu katika maeneo yote maana unapokuwa mvumilivu Mungu anakupa haki yako (Luka 18:7 – 8) katika shida yoyote au majaribu yoyote hata katika mahitajiyako yoyote unayotaka Mungu akutendee. Zidi kumwomba Mungu huku ukiwa mvumilivu usikate tamaa haraka maana Mungu ni mwaminifu kwa watu wote. Wavumilivu na wenye subira ni lazima watapokea yote sawa na maombi yao (Kol 1:10,11, Luka 18:7,8, Marko 11:22-24).3. UVUMILIVU SEHEMU YA IMANI YA MKRISTOImani inaambatana na uvumilivu. Mtu mwenye Imani lazima aambatane na uvumilivu (Ebr 6:12). Ibrahimu alihesabika ni mtu wa Imani kwa vile aliamini na vile vile alikuwani mvumilivu. Maana alijua yote aliyoahidiwa na Mungu, hata kama miaka mingapi ingepita ni lazima Mungu atayatenda (Warumi 4:16-22). Maana Imani ni kuwa na hakika ya mambo yasiyoonekana mambo yatarajiwayo (Ebr 11:1). Wana wa Israel kwa kukosa uvumilivu walisahau Mungu alivyowavumilia hatimaye wakamnung’unikia Mungu wakaharibiwa na Mharabu (1Kor 10:10, Hesabu 21:4-9). Ndiyo maana sisi wakristo tunapaswa kuwa wavumilivu katika yote yatakayotupata kwa ajili yaInjili (Rum 12:12-15, Kol. 1:10,11). Hata katika dhiki na udhia kwa uvumilivu wote inatupasa tuitendee kazi ya Bwana (2Tim4:5). Tunapaswa kuvumilia yote kama vile mkulima anavyo vumilia tangu wakati wa kuandaa shamba, kupanda mbegu mpaka zipate mvuaya kwanza na ya mwisho; nasi tuvumilie katika yote hivyo hatimae tutayaona mavuno yetu (Yak 5:7,8). Kumbuka vyakula vinapanda bei wakati wa njaa maana vyakula ndivyovinapandwa, kama mpunga, mahindi n.k; kama mtu asipokuwa mvumilivu akala mbegu zake ni hakika hatavuna chochote. Ndiyo maana kipindi cha kilimo ni kipindi cha kupanda kwa machozi lakini wakati wa kuvuna tutavuna kwa kelele za furaha (Zab 126:5-6, 2Kor 9:6-7, Ayu 4:8, Gal. 6:7). Kuteswa kwa ajili ya Mungu huo ndo wema hasa mbele za Mungu walatusibabaike bali tuzidi kudumu katika wokovu na kuitenda kazi ya Bwana. 1Petro 2:19. Tukiwa wavumilivu, ahadi zote nyingi tulizoahidiwa ni lazima tutazipata, maana Ibrahimu alizipata ahadi zote kwa uvumilivu (Ebr 6:13-15). Wote waliofanikiwa ni kwa sababu ya uvumilivu. Kumbuka Imani na uvumilivu ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa kila Mkristo aliye hai. Bibliainasema pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Ebr 11:6). Ayubu alikuwa mvumilivu hata katika mateso yaliyompatahakumkufuru Mungu ndiyo maana baada ya uvumilivu wake alikuwa ni mkuu sana alibarikiwa sana kuliko mwanzo wake (Yak 5:11, Ayu 42:12-17). Ndivyoitakavyokuwa kwa kila mtumvumilivu mwisho wa mateso, dhiki, adha unakuja.4. HASARA YA KUKOSA UVUMILIVUItakuwa vigumu kuona milango ya Baraka kufunguka kwetu kama hatuna uvumilivu. Ipo saa ambayo Mungu ameiweka kwa kila mmoja kupokea muujiza wake ila kinachotakiwa ni uvumilivu. Mtu aliyeokoka asipokuwa mvumilivu, Mungu atamuacha. Munguhatembei na wasio na uvumilivu. Wakati wa Nuhu, watu wengi walikosamiujiza wao kuingia katika safina kwa sababu ya kukosa uvumilivu, bali ni wanne tu ndio waliokoka katika safina (1Pet 3:20). Ndivyo ilivyo sasa, mtu yeyote aliyeokoka akikosa uvumilivu, siku ya mwisho atatupwa katika ziwa la moto (Math. 24:12-135. FAIDA YA KUWA MVUMILIVUMiujiza mingi na mikubwa Zaidi inapatikana kwa njia ya kuvumilia (Ebr 6:11,12, Isa. 40:31, Mith. 8:34). Mtu anayemsubiri Bwana ana heri. Maana yake amebarikiwa; maana hao ndio wanaoifanya kazi ya Bwana. Watu wa namna hiiwatazaa matunda kwa wakati wake, maana watazaa matunda kwa kuvumilia (Luk 8:15). Ikiwa hapa tunajifunza masomo mazuri Zaidi na kama hatuyatendei kazi kwa kutokuwahubiri wengine kwa kuwashuhudia, tutahesabika hatuna uvumilivu. Tukumbuke wavumilivu ndio wataopataBaraka nyingi (Zab. 37:9, Luk. 21:19, Math. 24:13).6. JINSI YA KUWA MVUMILIVUi. Kuhakikisha tumefanyika watoto wa Mungu kwa kutubu dhambi kwa kumaanisha na kuziacha.Yo. 1:12, Mith. 28:13, 1Yoh 5:18. Nivigumu mtu kuwa mvumilivu kama hajaokoka (Math. 13:20-21). Ndiyo maana ili tuwe wavumilivu ni lazima tuhakikishe tumezaliwa mara ya pili kwa kuokolewaii. Kudumu katika utakasoYoh. 4:7 kutokuwapenda ndugu, huo sio utakatifu; huwezi kumuona Mungu (Ebr 12:14). Upendondio utakaofanya kuwa mvumilivu 1Kor 13:17. Kila aliyeokolewa anapaswa aishi maisha ya utakatifu(Math. 5:48, 1Pet 1:15-16). Mwombe Bwana akutakase tena na tena kama maandiko yanavyosema kila mtakatifu na azidi kutakaswa (Ufu. 22:11)iii. Kuwa na kiu ya kumtumikia MunguKama mtu hana upendo wa Mungu, hatakuwa na kiu ya kumtumikia Mungu kwa hiyo hajapewa uvumilivu. Uvumilivu wanapewa watu kwa ajili ya kumtumikia Mungu,Isaya 44:3iv. Kumuomba Mungu kwa bidii yeye aliye shina la uvumilivu atuwezeshe kuwa wavumilivu Zab. 81:10, Kol. 1:

Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

SOMO: MWONGOZO WA KIBIBLIA WA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO

MADHABAHU. ZA KICHAWI ..KISHETANI~NA ZA KIPEPO ZA VUNJWA KWA DAMU YA YESU