JUA NINI MAANA YA UPAKO??
JE, NI NINI MAANA YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU?UPAKO WA ROHO MTAKATIFU(THE ANNOINTING OF THE HOLY SPIRIT)-Luka 4:16-22Kutiwa mafuta na Roho mtakatifu.Chanzo au asili ya Neno upako = kupaka, kumiminia.1. KATIKA AGANO LA KALEa. Kwa kiebrania = masah, limetumika mara 69, likiwa na maana ya kumiminia mafuta, kusambaza au kusiliba(kusibika) mafuta juu ya kitu au mtu anayepakwa.2. KATIK AGANO JIPYAa. Aleipho = limetumika mara 9 – karama tisa za Roho Mtakatifu?, likiwa na maana ya kupaka, kumiminia mafuta kwa lengo la au matumizi ya (a) kawaida (b) na ya kiibada.b. Krio=kazi maalumu, agizo maalumu – limetumika mara 5 katika biblia, huduma tano?) Luka 4:18; Mdo 10:38; 2Wakorintho 1:21; Waebrania1:9c. Chrisma-uwezo, nguvu; limetumika mara tatu katika Agano Jipya, likiwa na maana ya kutiwa naRoho Mtakatifu nguvu na uwezo Matendo 1:8, Pianguvu na uwezo wakuifahamu kweli na haki ili kuwa shahidi.i. Uwezo: ni kupewa;1. Kupewa moyoni hekima na ufunuo wa ufahamu, ulewa, na kujulishwa kusudi la Mungu2. Nguvu ya utendaji ulio sawa na kusudi au mapenzi ya Mungu.3. Ulinzi na kinga ya kimungu ya kutokwenda au kupatwa na lisilo kusudi la Mungu4. Zana au vitendea kazi vya kiroho na kimwili – vipawa na karama5. Anga la uweza, yaani eneo, milki, enzi au mipaka ya utendaji wa kusudi la Mungu6. Ratiba- muda na wakati wa utendaji wa makusudi ya Mungu.7. Nguvu kazi – watu au watenda kazi pamoja nawe katika kuyatimizamapenzi au makusudi ya Mungu.8. Kutetewa, kupiganiwa na Mungu.9. Kutiwa nguvu ya kusonga mbele bila ya kuchoka wala kukata tamakatika kumtumaini Mungu.3. MATUMIZI YA KAWAIDAa. Ni kama mojawapo ya vipodozi au manukato katika kuupendezesha mwili, (ngozi na nywele).b. Ni ishara au tendo la ukarimu kwa wageni au waheshimiwa wajapo nyumbani; au kwa viongozi na wafalme.c. Ni kuonyesha tendo la furaha au kufurahia ( kutokupaka mafuta ilikuwa ni ishara au alama majonzi au maombolezo)d. Ni dawa kwa tiba – fangasi, mba, koga, na vidonda. Luka 10:34; Isaya 1:6e. Ni dawa ya kutunzia maiti isioze – yalichanganywa ili kufanya manukato ya kuletea mwili hali ya kutooza.4. MATUMIZI YA KIIBADAa. Kuvipaka vitu vya kiibada(vya kuabudia), mfano: madhabahu, vyombo vya ibada, Mwa 28:10-18, Kutoka 30:26-29, Walawi 8:10-11b. Kuwapaka watumishi wa Mungu wa Kidini(wanadhiri, makuhani, manabii) na Kiutawala-serikali(wafalme); na hivyo waliitwa wapakwa mafuta wa BWANA (Kiebrania=masah,yaani messiah/masihi, na Kiyunani/kigiriki = Kristo) 1Samweli 10:1; 16:13.c. SABABU KUU YA KUPAKA MAFUTAi. Ni kuweka wakfu (kuchaguliwa, kutengwa au kuteuliwa kwa kazi maalumu tu)ii. Kuonyesha ishara ya kupewa AGizo au kazi maalumu (appointment) ya Mungu.iii. Kuonyesha ya kuwa umepewa mamlaka au uwezo maalumu kwa kazi maalumuya Mungu.iv. Kuhalalisha kwa kazi maalumu na si kwa kazi nyingine.d. KUWEKA WAKFU (CONSECRATION)i. Kuweka wakfu ni kutenga au kuweka rasmi au kuweka maalumu kando kwa ajiliya matumizi matakatifu kwa kusudi maalumu la Mungu na wakati maalumu unaokubalika mbele za Mungu.ii. Ni ishara ya Mungu kukipa chombo uhalali na mamlaka ya kutumika kwa ajili yakusudi maalumu na kwa wakati maalumu ulliokubalika na Mungu (siyo chombo chenyewe!)iii. Ni ishara ya kuwa chombo hicho kitumike na Mungu na kwa kazi yake maalumutu, hivyo asikitumie mwingine au kwa kazi nyingine!iv. Ni chombo kufanywa cha kufaa kwa ajili ya Mungu.v. Ni wito maalumu wa mungu kwa mtu kwa ajili ya kazi maalumu, wito maalumuunaowekwa wazi kwa wote kwamba umetoka kwa Mungu!vi. Ni udhihirisho wa hadharani wa kuonyesha chaguo loa Mungu kwa ajili ya Mungu mwenyewe.vii. Ni uwakili, kuchaguliwa, kuteuliwa, kuitwa.viii. Kuonyesha kuwa ameteuliwa(mteule, mtumishi) au masihi, kristo.ix. Kuwa mtumishi wa huduma ya kiroho; mfano: Kuhani, nabii, au mkristo wa kweli!x. Kuwa mtumishi wa huduma ya kiserikali, mfano: mfalme, raisi, na raia mwema!xi. Ni kuonyesha uwepo wa Roho Mtakatifu na uponyaji wa kiroho na kimwili.e. KANISAi. Ekkaleo=(Ek=kutoka, Kaleo=ninaita) walioitwakwa wito maalumu kutoka/kutengwa kwa ajili ya jina lake; yaani kusudi lake maalumu la wakati maalumu, kwa namna maalumu, na kwa wakati uliokubalika na Mungu.ii. Ekklesia = kusanyiko maalumu la watiwa mafuta wa Mungu(wakristo); yaaniwenye upako wa RohoMtakatifu!iii. Kurriake = waliotengwa kwa ajili ya Jina lake(yaani kwa ajili ya kazi yakemaalumu na kwa wakari maalumu uliokubalika na Mungu!)iv. Wokovu ni wito maalumu, kwa wakati maalumu, kwa kusudi maalumu, na kwanamna maalumu iliyokubalika na Mungu (2Wakorintho 6:2; Warumi 8:28-30)v. KUPEWA AGIZO, KAZI MAALUMU(appointment, assignment, commission=tume,kutumwa;vi. Kupewa agizo au kazi maalumu kwa wakati maalumu uliokunalika(sio kuwahi,wala kuchelewa) kwa ajili ya kusudi maalumu la mungu.vii. Kuwekewa kazi maalumu ya kuifanya; mfalme? Kuhani? Nabii, mchungaji, mwalimu, mkristo muhudumu? – Mathayo 28:18-19;viii. Kugawiwa mamlaka, amri, juu ya eneo maalumu la kazi maalumu na kwa wakatimaalumu.f. KUPEWA UWEZO/NGUVU kwa ajili ya kazi maalumu na wakati maalumu, uliokubalika.i. Ni Mungu kuwekeza nguvu zake (talanta), uwezo wake ndani ya mwamini ili azitumie kuzalishia kwa ajili ya kazi yake.5. MAANA YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFUa. Ni nafsi na uwepo wa Roho Mtakatifu katika kutusaidia kuyatambua na kuwa na uwezo wa kuyatimiza makusudi au mapenzi ya Mungu yaliyo katika moyo wa Mungu, ili kumpendeza Mungu; kama Daudi na BWANA YESU KRISTO walivyoupendezaMoyo wa Mungu.b. TABIA ZA MTU MWENYE UPAKO AU ALIYEJAAUPAKO!i. KUITWA/ WOKOVU – kutambuliwa, kuitwa, kukubaliwa, kuteuliwa na Mungu;anakuwa ni mtu mwenye wito maalumu kwa kusudi maalumu la Mungu; hivyokupata kibali mbele za Mungu na wanadamu(japo si wote), yaani, kumpendezaMungu na wanadamu wenye mapenzi mema; anakuwa ni mtu mwenye kumpaMungu utukufu wote, na wanadamu wanakuwa na amani nawe! Luka 2:52.ii. WITO ni sauti isikikayo moyoni mwa mtu kwa:1. Nia ya moyoni ya kumpendeza Mungu2. Moyo wa kupenda, wa hiari, kupendezwa3. Msukumo au mguso wa moyoni4. Kukereketwa moyoni na kushindwa kutulia kwaajili ya mambo ya Mungu.5. Wivu wa moyoni kwa ajili ya mambo ya Mungu.6. Kiu, njaa, na hamu ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu na utukufu waMungu tu!iii. KUJAZWA AU KUPEWA NEEMA-Kuwezeshwa, kupewa nguvu, kutumiwa na Mungu na kupata ushindi au kufanikiwa (kuwa na uwezo maalumu)Warumi 8:31-39; Sababu:1. Anatenda lililokududiwa kwa kusudi na mapendi ya Mungu2. Lililo kwa wakati wa Mungu3. Mahali alipopakusudia Mungu4. Kwa wakati alioukusudia Mungu5. Kwa namna ile aitakayo au aliyoikudusia Mungu6. Kwa nguvu zisizopingika za Mungu7. Lililo kwa uongozi wa Roho Mtakatifu – si kwa uwezo,wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho … Zekaria 4:6.iv. KUTUMIKA – kuifanya kazi maalumu ya Mungu inayodhihirika kwa matokeo yake mazuri kwa Mungu, kanisa, na kwa watu wengine; Agizo maalumu. Huduma mbali mbali (Warumi 12:3-21)kwa mfano: kushuhudia, kuhubiri,kufundisha, umisheni, utoaji, maombi na maombezi, huduma kwa wasiojiweza…
Comments