UMUHIMU WA KUSAMEHE KWENYE MAOMBI YAKO INAAYO HUSIANA NA KUJIBIWA
Muhimu katika Kusamehe. 3. SAMEHE NA KUSAHAU: Wakati fulani nilikuwa mahali nikifanya semina ya neno la Mungu. Mtu mmoja akanifuata na akaniambia anataka nimuombee. Nikamuuliza; “Nikuombee nini?” Akasema; “Mimi shida yangu ni kwamba naona imani yangu ni ndogo na haikui, na maombi yangu hayajibiwi. Kwa hiyo naona nina shida katika maisha yangu ya kiroho, uniombee “. Inawezekana hata wewe una shida ya namna hiyo, kwa hiyo tafakari kwa makini maneno haya. Niliahidi kumuombea baadaye kwa maana muda ulikuwa umekwisha. Siku moja nilipokuwa ninaomba kwa Mungu juu ya shida yake, Bwana akanijibu katika roho yangu kuwa: “Mtu huyo ana matatizo ya ndoa na kuna jambo lililomuudhi. Yeye anafikiri amesamehe, lakini bado ana uchungu moyoni mwake. Mwambie asamehe na kusahau na shida yake itakwisha”. Nilipowasiliana naye juu ya jambo hili, alikubali kuwa, ni kweli mwenzie amekuwa akimkosea mara kwa mara katika ndoa yao. Lakini alisema amekwisha msamehe. Nikamuuliza; “Je! mbona basi kila mkikosana unakumbusha makosa ya nyuma?” Akajibu; “Ni kweli, sasa nifanyeje wakati naona kila wakati makosa aliyonifanyia nyuma yakinijia kichwani?” Hili ni tatizo la wengi. Na hujikuta wanasema wamesamehe kumbe bado. Msamaha si jambo la akili ni hatua ya rohoni. Ni uamuzi unaotoka ndani ya moyo wako. “Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, sikuambiii hata mara saba, bali hata saba mara sabini ” (Mathayo 18:21, 22) “Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba , akisema, nimetubu msamehe. Mitume wakamwambia Bwana tuongezee imani” (Luka 17:4,5). Mistari hii inatuonyesha jinsi kukua kwa imani, kunavyohusiana sana na kusamehe. Wanafunzi walimwambia Bwana Yesu, awaongezee imani. Kwa kuwa walifahamu kwamba, kwa uwezo wao wasingeweza kusamehe kama Kristo anavyotaka. Ni kweli kabisa. Kama vile unavyohitaji imani katika kuomba, vile vile katika kusamehe na kusahau unahitaji imani. Ulipompokea Kristo ulipokea kiasi cha imani (Warumi 12:3) Na ili iongezeke unahitaji kusoma neno la Mungu na kulitenda. Imani huja kwa kusikia Neno la Mungu. (Warumi 10:17). Imani ni ya rohoni na kusamehe ni kwa rohoni. Unawezaje kusamehe na usiyakumbuke uliyofanyiwa? Hilo ndilo tatizo kubwa alilokuwa nalo yule mtu aliyeniambia niomuombee. Na wengi pia wana tatizo la namna hii, na limekwamisha uponyaji na majibu mengine ya maombi yao, wameombewa mara nyingi, lakini bila mafanikio. Kusamehe na kusahau ni kitendo cha imani ambacho ni budi kionekane kwa njia ya matendo ya mtu. Kusamehe ni uamuzi wa mara moja na kusahau ni vita vya imani. Sasa, utaniuliza, Ndugu Mwakasege, utawezaje namna hiyo? Kabla sijakujibu, na mimi nakuuliza swali. Siku ulipotubu dhambi zako, ulikuwa na uhakika gani ya kuwa Mungu amekusamehe wala hazikumbuki dhambi zako tena? Utasema kwa kuwa ukitubu Mungu anasamehe. Ni sawa kabis
Comments