DAMU NI NINI?
MAMBO YA WALAWI 17;11 ; kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu;nami
nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu,ili kufanya upatanisho kwa
ajili ya nafsi.zenu,kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya
nafsi .
Biblia inatuonyesha kwamba uhai wa mwili uko ndani ya Damu. Tena damu
ndio inaleta upatanisho wa nafsi. Hakuna uhai katika mwili bila damu pia
hakuna uhusiano katika mwili na nafsi pasipo damu.
Damu inaleta uhai kwenye nafsi . ina maanisha kwamba kiroho kuna uzima
wa kiroho kwa njia ya damu . ulimwengu ambao ulikufa na kupotea hata
kuzama katika maovu na kufungwa kwenye minyororo ya shetani ulikuja pata
tena uhai na kupatanishwa kiroho kwa nguvu ya damu ya Yesu kristo. Ni
damu ya yesu kristo inapatanisha ulimwengu (mwili) na Mungu (roho na
nafsi). Soma ;Waefeso 2;12-13.
DAMU YA YESU KRISTO NA KAZI ZAKE
Damu ya yesu kristo ina kazi ya ajabu kwa maisha yetu wanadamu. Ni kwa
njia yake ndio sisi tumeokoka ,tumepona, tumekombolewa na kuitwa tena
viumbe hai na huru. Hii Damu inafanya kazi zifuatazo ;
1. INATUPATIA UZIMA WA MILELE
Yohana 6;53-56
Msipoula mwili wake mwana wa Adamu na kuinywa damu yake hamuna uzima
ndani yenu.
Tunapata uzima kupitia Damu ya mwana kondoo yesu kristo. Sisi ambao
tulikua wafu ajili ya dhambi zetu tumepata uzima mpya kwa njia ya damu
yake . Waefeso 2;6,Yakobo 3;15,16; 1 petro 1:4.
2. INAMFANYA YEYE AKAE NDANI YETU NASI NDANI YAKE
Yohana 6:56.
Kukaa ndani yake nayeye ndani yetu ina maanisha kuwa na uhusiano bora
naye. Kuwa na urafiki wa karibu sana katika maisha yetu kila siku na
saa.
3. IMETUNUNUWA
1 Wakorintho 6:19-20, Waroma 12:1-2
Tumenunuliwa na kufanywa hekalu la Mungu kwa njia ya damu ya yesu
kristo. Miili yetu sasa sio yetu tena bali imekombolewa kutoka kwa
ulimwengu na kufanywa ya kumtumikia kristo. Ndio ibada takatifu hiyo.
4. ILIOSHA DHAMBI ZETU
Ufunuo 1:5; 1Yohana 1:5
Ni damu ya Yesu pekee ndio inatuosha maovu na dhambi zetu na kutufanya
safi hata kutuweka kwenye nuru yake Mungu mwenyezi.
5 .IMETUFANYA WENYE HAKI
Waroma 5:9 ;1KOR 5:7; Hebr 10:29, 13:12.
Kupitia Damu ya Yesu kristo tunahesabiwa wenye haki na kupata Baraka
zote za wenye haki. Hatuhesabiwe tena hukumu juu ya maovu. Tunaepuka
hukumu ya Mungu nakuingia kwenye ahadi zake. Kwa hiyo tuna pata:
amani,furaha,salama na kuridhi haki za watoto wa ufalme wake.
6. IMETUTAKASA NA KUTUFANYA WATAKATIFU
Hebr 13:12
Nidamu yake ndio inatufanya watakatifu na kutuosha maovu yote.
Tunaikimbilia kupata utakatifu na kutufanya safi bila mawaa yoyote wala
dosari.
7. INATULETEA MSAMAHA WA DHAMBI ZETU
Math 26:28, Ef 1:7
Dhambi za kale ,za wakati wa sasa na unaokuja zimesamehewa na Mungu
kupitia ile damu ya mwana kondoo yesu kristo. Hebr 9:12,28, 10:10.
8. IMEOSHA DHAMIRI ZETU
Hebr 9:14
Mambo yote ambayo muovu aliweka kwenye dhamiri zetu, kuzipofusha na
kutia giza ndani yake Damu ya yesu iliosha na kusafisha hata kufanya
dhamiri zetu kuwa safi na kumujua Mungu aliye wa kweli na mtakatifu.
Tumefanana na Mungu mtakatifu kwa dhamiri zetu kwa njia ya damu ya mwana
kondoo Yesu Kristo.
9. IMETUPATIA UJASIRI WAKUPAINGIA PATAKATIFU
Hebr 10:19-23
Mshahiri huu unatuonyesha namna gani tunapata ujasiri wa kuingia
patakatifu pa Bwana kupitia damu ya yesu kristo. Pasipo damu ya mwana
kondoo hakuna yeyote angekua na uwezo wakuingia patakatifu wala
kumkaribia Baba wa mbinguni. Tunajipigia kifua damu ya yesu kristo.
10. INATUPATIA USHINDI NA MAMLAKA ZIDI YA NGUVU ZA SHETANI NA PEPO ZAKE
2 Kor 2:1-5 ,Uf 12:11, 2 Kor 10:3-5
Tuna mamlaka na nguvu ya kushinda nguvu za shetani na pepo zake kupita
nguvu ya damu yake yesu kristo. Woga unaondoka ,mashaka yanaondoka,
natunatiwa tumaini na imani yetu kuongezeka ndani ya nguvu ya damu ya
yesu kristo. Nguvu hii tuliyo nayo siyo ya mwili bali ni ya roho maana
damu ya yesu kristo inatumika ndani yetu kiroho na kutenda kazi kiroho
ndani ya maisha ya kiroho na ufalme wa kiroho pia.
11. INATUPATANISHA NA KRISTO
Ef 2:13-14
Damu ya yesu kristo imetufanya umoja nakutupa amani . sisi tuliokua
tumetengana na kristo ,kwa njia ya damu yake tena tumemkaribia. Ile damu
imebomowa kuta za matengano nakutufanya watoto wa baba moja. Hakuna
mzungu tena na mweusi wala mufaransa na mungereza ,sote tumeitwa watoto
ndani ya nyumba moja ya baba wetu. Hatuitwe tena vikundi vikundi bali
kikundi kimoja cha watakatifu waliokombolewa na kununuliwa na kuokolewa
kwa damu . Mungu amejinunuliya wote wakawa wake kwa damu ya yesu.
Haya ndiyo mambo yanayo tuonyesha kwamba damu ya yesu kristo ndio
yenyewe inatuokoa na kutukomboa pia. Hakuna shaka kusema kwamba bila
damu ya yesu hakuna wokovu. Wokovu sio kwenye dini, wala mtu awaye yote
bali ni kwanjia tu ya yesu mwenyewe .
Wala hakuna wokovu katika mwengine awaye yote ,kwa maana hakuna jina
lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo Mdo 4:12
Bwana awabariki sana.
Amen.
Comments