GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA HIZI HAPA

*1⃣SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA  MOROGORO  SEKONDARI*
*MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE*
*SOMO: FAIDA ZA KUOMBA KWA KUNENA KWA LUGHA*
*SIKU YA KWANZA JUNE 14, 2017.
Kitabu cha Hongera kwa kuokoka   https://drive.google.com/file/d/0BxdP6mgDJWByVERtampLTGZWRms/view?usp=drivesdk
Semina iko  live  kuanzia saa kumi jioni kwa njia zifuatazo.
1.Radio Sauti ya injili (Moshi, Arusha,Tanga,Dsm,Morogoro,Manyara,Kusini mwa Kenya na Pemba)
2.Redio starter  ya Njombe
3.Redio Hhc alive (Mwanza)
4.Redio Baraka Fm (Mbeya)
5.kwa njia ya mtandao tembelea www.mwakasege.org utapata maelezo pale.
*MALENGO YA SOMO*
1.Zijue faida za kuomba kwa kunena kwa lugha ili uweze kuomba kwa imani kwa kunena kwa lugha.
2.Ujazwe Roho Mtakatifu ili uweze kunena kwa lugha
Matendo ya Mitume 2 :4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
1 Wakorintho 14 :5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.
*MAMBO MATATU YA UTANGULIZI*.
1.Kunena kwa lugha maana yake nini, kufuatana na Matendo 2:4 maana yake ni kuongea kwa lugha nyingine ambayo Roho Mtakatifu aliwajalia kuongea. Au kusema lugha usiyoijua kwa msaada wa Roho Mtakatifu
1 Wakorintho 14 :2-15 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake. 14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. 15 Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.
Paulo anaandika kuwa  ataomba kwa akili maana yake ataomba kwa kuelewa kile ninacho omba. Ina maana akiomba kwa lugha ina maana haelewi hadi afasiriwe.
Pia katika kunena kwa lugha kumbe sio unaomba tu bali kuna kuimba pia kwa lugha.
2.Roho Mtakatifu anaweza kukuongoza kusema lugha za wanadamu na za malaika
1 Wakorintho 13 :1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
Kumbe mtu anaweza kunena kwa lugha hata za malaika na ndivyo tunaona kwenye biblia. Mtu anaweza pia kunena kwa lugha za wanadamu huku duniani.maana kuna lugha nyingi sana mfano hapa nchini kwetu Tanzania tuna lugha zaidi ya 120 za makabila tofauti tofauti.
            Kiswahili sio lugha ya kabila lolote ni lugha ya kitaifa na imechukua maneno kutoka lugha tofauti tofauti, Mfano tukienda ujerumani neno shule hata kule ni shule hivyo hivyo. Tulienda Israel na tulikutana na waraabu na walishangaa kuona na sisi tunahesabu 40 na 30 na 50 na wakajua ni kiarabu ila tuliwaambia hapana ni kiswahili walishangaa sana.
  siku moja nimeenda kufanya ziara uingereza na Ireland na ndipo nilijua kuwa kumbe sio wote ni waingereza na nilishangaa kuona na wao wametunza lugha za makabila yao maana nilienda hadi vijijini  na wakawa wananiambia hapa ni kabila fulani.
3.Kuna  tofauti kati ya kunena kwa lugha kama karama na kunena kwa lugha kwa kila aaminie.
_1 KOR. 12:4‭-‬11‭, ‬28‭-‬31 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.   Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora._
_Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;_
 Tumeona  katika 1Wakorintho 14:5a Paulo akisema nataka ninyi nyote mnene kwa lugha mpya  ni huyo kaandika katika ile sura ya 12 ya kuwa ni karama ambayo mtu anapewa. Nimesema hii maksudi maana  kuna wengine hawatataka kunena kwa lugha au watasingizia kuwa sio karama yao.
   Kuna tofauti ya karama ya aina za lugha na tafsiri. Karama ya aina ya lugha Mungu anakupa kusema lugha yao. Na Mungu anafanya hivyo ili watu unaozungumza nao waweze kuelewa, na sio mara nyingi inatokea.
  Mimi ilinitokea mara moja tu nilipoenda kijijini kuhibiri kinyakyusa kule Tukuyu na mimi ni mnyakyusa nilieondoka mwaka 1965 na huwa naenda mara chache. Baba yangu alikuwa ni mchungaji na nilienda kule wakati wa likizo akaniambia Bwana mdogo utahubiri kanisani. Akasema ila utahubiri kwa kinyakyusa na akaniambia kule hawaelewi Kiswahili. Akanipa biblia ya kinyakyusa ya agano jipya “utestamenti umpya” na nilisoma sikuelewa basi nika andaa mahubiri kwa kiswahili na nikawa naomba sana Mungu anisaidie ili niweze kueleweka kwa wale watu. Baba yangu alikuwa anaongoza ibada na akawatangazia kuwa leo Bwana mdogo atahubiri. Saa ya mahubiri nilimpa baba ile biblia ya kinyakyusa asome na wakati anasoma nikawa naomba kimoyo moyo na nikafungua mdomo na kiswahili kimepotea. Nilihubiri kinyakyusa kwa saa moja hivi na nikawaita hadi watu kuokoka na nikawaongoza na sala ya toba kwa kinyakyusa.
  Tulipomaliza baba yangu alisema we si ulisema hujui kinyakyusa mbona sasa umeongea nikamwambia kile sio cha kwangu (maana nilisaidiwa na Roho Mtakatifu kuongea).
   Inapokuja kunena kwa lugha kwa kila aaminiye na Paulo anatutia moyo kuwa watu wanene kwa lugha na yeye anasema anajua faida ya kufanya hivyo ndio maana alisema mimi nanena kuliko ninyi nyote.
  Ile kwamba hupati mafundisho katika kanisa lako haina maana hayapo ndani ya biblia. Kwa hiyo usijaribu kusema hicho sio cha kwetu ni cha kanisa lingine. Sasa sio hivyo maana hilo kanisa lingine limedaka haraka na kulifanyia kazi. Kwa hiyo usiseme sio ya kwetu wakati ipo kwenye biblia. Lazima ujue wapi pa kunena na wapi pa kunyamaza maana biblia inasema mambo yote yafanyike kwa utaratibu.
   Wewe fikiria umeambiwa uombee chakula na unaanza laba…. Uwe na uhakika baada ya kusema hivyo wenzio watakuwa wamemaliza kula. Labda iwe ni dharura Roho Mtakatifu anakuambia uombe ndio ufanye hivyo, ila ile kunena kwa lugha ili uonekane ni wa kiroho hilo ni jambo lingine sasa.
*FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA*
Hizi faida nimeziweka tu randomly ile ya kwanza haina maana ndio ipo hivyo kwa mpangilio wake mmmmmh sio hivyo.
1.Kuongeza kiwango cha nguvu zitendazo kazi ndani yako zinatozumika kujibu maombi yako.
_WAEFESO. 3:20 Basi  atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;_
Neno kadri linaonesha kipimo au kiwango ina maana imekadiriwa.Roho Mtakatifu huwezi kumpima ila nguvu zake zinapimika.daka hiyo itakusaidia. Huwezi kumuweka Roho Mtakatifu kwenye box na ukapima kilo yake lakini nguvu zake zinapimika.
  Lazima ufahamu hilo maombi au mawazo yaliyokaa katika mfumo wa maombi, Mungu anatujibu maombi yetu kwa kadri ya nguvu za Mungu zinazotenda ndani yako
  Kwa lugha nyingine ni kuwa huwezi kujibiwa maombi zaidi ya utendaji wa nguvu zilipomo ndani yako. Na ukiangalia tena hapo unaona kiwango cha utendaji wa nguvu ndani yako kinategemea gharama uliyo tayari kugharamia ili kuhakikisha hiyo nguvu inafanya kazi.
   Ni mambo ya msingi unahitaji kufahamu.kama una umeme nyumbani kwako kunagharama kuu mbili. Ya kwanza ni gharama ya kuingiza umeme (wiring, service charge) na wataangalia ni umeme wa phase ngapi ili wakushauri aina ya umeme na watakushauri hata switch za kutumia maana matumizi yanaweza yakawa makubwa. Na wanakuwekea na mita au Luku.
    Mita watakuja kusoma umeme uliotumia watakuandikia bill na utalipa. Luku unakadiria umeme utakao utumia na unalipa kabla. Ukiisha inakata, sasa inategemea wewe unataka kuingia gharama kiasi gani. Sasa ukitaka kutumia mwanga mkubwa ni uwe na bulb nyingi au moja kubwa lakini lazima itumie umeme mwingi. Sasa watu wengi sana wanasema huu umeme unakula pesa nyingi sana tumia bulb ndogo. Sasa sio kwamba huna umeme bali ni aina ya matumizi uliyoyachagua wewe mwenyewe.
   Utapata mwanga kwa kadri ya utendaji kazi wa kile chombo kinachotumia na sio kwa kiwango cha umeme uliopo ndani yako. Maana kama taa ina watt 40 utapata kwa kiwango hicho na wa watt 120 nae atapa kwa kiwango chake.Tofauti yenu ni kwenye kifaa kinachotumia umeme.
   Sasa sikia umeme usiotumia hauna faida kwako na kwa TANESCO. Nguvu za Roho Mtakatifu ulizonazo kwako na hazitumiki hazina faida kwa Mungu, kwako na kwa ufalme wake.
    Watu wengi wanataka kuombewa upako (nguvu za Roho Mtakatifu) na kujua na sio unakuja kama mapambo na hufanyii kazi. Ndio maana utaona mtu anaombewa na nguvu za Mungu zinashuka na huzifanyii kazi na utaona baada ya semina upako unaondoka na kubaki wa kawaida.  Na sababu ni kuwa hujaufanyia kazi  ndio maana umeondoka kwako. Nguvu za Roho Mtakatifu zikikujia inabid uzifanyie kazi.
Na ukienda katika biblia Roho Mtakatifu anakuja saa unapo okoka anakuwa chemchem ndani yako na ndivyo Yesu alimwambia yule mama msamaria kuwa chemchem zitatoka ndani yake. Sasa ukijazwa nguvu ndani yako ile chemchem inageuka na kuwa mito (maana Saiz ya kisima chako kinaongezeka). Kazi ya chemchem na kazi ya mito ni vitu tifauti.
 Kuna watu saa wanaokoka hawajazwi Roho Mtakatifu hapo hapo na wengine wanajazwa Roho Mtakatifu saa wanaokoka hapo hapo
_Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi? Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha. MDO 10:44‭-‬48_
Walikuwa hawajaokoka na walijazwa Roho Mtakatifu na kubatizwa .
Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.MDO 19:1‭-‬6
Hawa ndugu walikuwa wameokoka kabisa ila hawaeni kwa lugha na hapo tunaona Paulo aliwasaidia ili waweze kunena kwa lugha.
 Pia ukiangalia Nyumbani kwa Kornileo watu walinena kwa lugha na walikuwa hawajaokoka wala kubatizwa. Na tunoana watu wa Efeso walibatizwa ndipo walinena kwa lugha. Sasa kwanini tunajifunza mambo haya ni ili tuone neema ya Mungu  maana hauhitaji kuweka mipaka  ya kiwango cha nguvu ndani yako.
  Hakikisha una kiwango cha nguvu ndani yako cha kutosha, na lazima uende  kama maandiko yanavyosema Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; EFE. 5:18. Katika biblia ya kiingereza anasema mjazwe nguvu kila siku. _And do not get drunk with wine, for that is debauchery; but ever be filled and stimulated with the [Holy] Spirit. [Prov. 23:20.]Ephesians 5:18 AMPC_
Unapoomba ujaza nguvu na unapotumikaa unatoa nguvu
_Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma. Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga. *Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka*. Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara. Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani.LK. 8:43‭-‬48_
 Ukisoma Marko anazungumza kitu cha ajabu sana anasema  30 *Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka*, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?  Marko 5 :30
Na ile Luka 22:40-43 Yesu alipokuwa anaomba na Malaika akaja kumtia nguvu kutoka mbinguni. Kwa hiyo unatembea katika Mungu  (Pasipo Mungu hatuwezi kufanya lolote) ina maana mafuta ya Roho Mtakatifu yanatumika na yanatoka na kupunguza na ndio maana inabid uende kwa Mungu akutie nguvu tena
Mtakeni Bwana na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote.(1 Mambo ya Nyakati 16:11,Zaburi 105:4).
Sasa tuje kwanini Malaika alikuja kumtia Yesu nguvu ni kwa sababu alikuwa anatumia nguvu zilizokuwa ndani yake kabla hajamaliza kuomba. Sasa kwa jinsi ya kibinadamu. Tungesema kuwa kwanini basi Mungu kwa jinsi ya kibinadamu asimsaidie tu mtoto wake. Tunajifunza kuwa katika ulimwengu wa Roho Mungu kuna utaratibu kauweka wa kutumia nguvu za mtu zilizo ndani yake. Sasa mara chache Mungu anaachaa kufuata utaratibu na ndio tunaita muujiza.
Unapomba na ukajazwa nguvu za Roho Mtakatifu na ishara mojawapo ni ya kuzungumza kwa lugha mpya. Kama kufanyii hivyo ina maana nguvu zipo kwa kiwango fulani.  Na katika kipindi cha kiangazi ndipo tunaona ya kuwa mabwana yanakuwa na maji kiasi fulani yaani yamepungua sio kwamba hayana maji. Na kwa maana hiyo tunaona kunakuwa na mgao wa umeme.
Sasa sijajua kwako Mungu amekuwekea nguvu za kiasi gani  na injini ya kiasi chako, na hata tanki zinatofautiana. Kwa hiyo lazima urudi kwa Mungu ili akujaze tena nguvu na ili injini ifanye kazi. Na unapokuwa unanena kwa lugha nguvu ndani yako zinakuwa zinajaa  na kufanya kazi na kuachilia ujibiwe maombi yako.
Na tunaona Elia alivyoomba wakati anataka mvua na akaomba na akachungulia na akaomba tena hadi mara ya saba hadi aliona wingu. Nguvu alizotumia kuomba kutengeneza mazingira. Na ukinena kwa lugha unaona nguvu zinaongeza na hali ya hewa inabidilika. Kwa hiyo kama huneni kwa lugha omba Mungu akusaidie unene kwa lugha maana hii ni kipawa na kipawa maana yake ni zawadi hii tunapewa bure. Ila karama ni kitendea kazi Mungu anatoa kwa ajili ya kazi.
Kunena kwa lugha sio passport  ya kwenda mbinguni  maana unaweza ukaokoka na usinene kwa lugha na mbinguni ukaenda. Ila kunena kwa lugha kuna faida sana kwa mtu hata akiwa hapa duniani maana unaongezewa nguvu.
Kwa hiyo maandiko yanasema mtakeni Mungu na nguvu zake kila siku sasa lazima jifunze kwenda “Petrol station” kwa ajili ya kuongezewa mafuta ya Mungu ndani yako. Maana utaona kuwa  kama nguvu za Mungu zimeisha ndani yako ina maana umetumika sana na hujaongeza nguvu. Omba kwa kunena kwa lugha ili ujenge nafsi yako (ujaze mafuta yako).
Ili upate hizi nguvu lazima uingie gharama maana kadri unavyoingia ya kwende mbele za Bwana nguvu zako ndio zinaongezeka na gharama nyingine ni kukubali kuokoka. Nilienda mahali  nikawaambia watu wanaotaka kujazwa Roho Mtakatifu wasimame wakasimama wengi. Nikasema kama unataka hizi nguvu lazima uokoke na kama unakata kuokoka simama na hutaki kuokoka kaa chini,  kuna wengine hawakutaka kuokoka wakakaa chini na waliotaka kuokoka ili wapate double na wakasimama.  (Haya mambo yanashangaza sana mtu hataki kuokoka na anataka nguvu za Mungu, usifanye kosa la namna hiyo hakikisha unaokoka kama hujaokoka ili nguvu za Mungu zijae kwako na kukusaidia  au uliokoka ukarudi nyuma hakikisha unatengeneza na Mungu)
Wewe ambaye umeokoka kwa mara ya kwanza au unataka kuokoka hakikisha unaokoka na unampata Yesu. Na soma kitabu cha Hongera kwa kuokoka.
Pia angalia link pale juu utapata somo zuri la utangulizi ka kukusaidia.
Ili usome vizuri hicho kitabu hakikisha unakuwa na application ya google drive kwemye simu yako.
Mbarikiwe na Yesu.
  ==Glory to God Glory to God ==


Comments

Popular posts from this blog

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

ondoa jiwe iliujibiwe maombi yako