MAFUNDISHO
YA SEMINA YA MWALIMU MWAKASEGE
AKIFUNDISHA KUHUSU FUNGUO ZA MBINGUNI.
“Nami nakuambia ….. na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala
milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na
lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:18 – 19).
Maneno haya ya Yesu Kristo yanatuonyesha kuwa, nia yake ni kulijenga kanisa
lililo na mamlaka kuliko shetani. Kanisa ni mwili wake (Waefeso 1:22 – 23).
Wakristo waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo ni viungo vya mwili wa Kristo –
ni viungo vya kanisa (1 Wakorintho 12:12, 13, 27). Kwa hiyo Yesu Kristo
anaposema atalijenga kanisa lake wala milango ya kuzimu haitalishinda – ana
maana ya kuwa, kila mkristo aliye wake anajengwa kiroho awe na mamlaka ya kumshinda
shetani.kwenye kila majaribu unayo pitia
hata kama ni magumu kiasi gani.
Ni budi tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufungue kama hakuna
kitu cha kukifungua. Hawezi kutuambia tufunge kama hakuna kitu cha kufunga. Kwa
hiyo ni lazima kuna vitu vya kuvifunga na kuna vitu vya kuvifungua.
Pia, tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufunge na kufungua kabla
hajatupa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo. Uwezo na mamlaka tunapata ndani ya
Kristo aliyetukabidhi funguo za ufalme wa mbinguni.
Itakuwa haina maana kwa Yesu Kristo kutukabidhi funguo bila ya kutufundisha
namna ya kuzitumia. Hawezi kutukabidhi mamlaka bila kutufundisha namna ya
kuyatumia.
Yesu Kristo anasema tukifunga au tukifungua, mbinguni nako kunatia mhuri
kitendo hicho. Hatuwezi kufanya hivyo kama tulichokifanya hakifanani na mapenzi
yake. Ndiyo maana tunaomba kuwa mapenzi yake yatimizwe hapa duniani, kama
yanavyotimizwa huko mbinguni. Kwa maneno mengine tunaweza kusema ya kuwa
ukifanya kitu chochote katika mapenzi ya Mungu, Ufalme wa mbinguni utakuwa
upande wako.
1.
Aina za Funguo:
Biblia inazungumza juu ya funguo za aina tano zifuatazo: kama
zifuatanzo na ukizisoma kwa makini na kuziweka kwenye matendo utauona mkono wa
bwana ukikuonekania maishani kwako mote
na wala milango ya kuzimu haitakushinda
1. Funguo za Ufalme wa Mbinguni – Mathayo 16:19 – Yesu Kristo amekabidhi funguo
hizi kwa wakristo (Kanisa).wote katika kanisa sasa usipo zitumia shetani
atazitumia badala yako
2. Funguo za mauti na za kuzimu – Ufunuo 1:18 – Funguo hizi anazo Yesu Kristo –
baadaye atampa Malaika mmoja funguo za kuzimu ili amfunge Ibilisi (Ufunuo
20:1-3).
3. Ufunguo wa nyumba ya Daudi – Isaya 22:22; Ufunuo 3:7. Ufunguo huu anao Yesu
Kristo.
4. Ufunguo wa kawaida wa mlango – Waamuzi 3:25.
KUMBUKA
BILA FUNGUO HAUTA WEZA KUFUNGUA BARAKA ZAKO AMBAZO ZIMEFUNGWA NA SHETANI
Comments