GRACE OF GOD

Image
  THE FOLLOW IS THE STEPS ON HOW  GOD TO HELP YOU Step 1: Be awake to God’s Word to yo Truth:  God’s Word has the answers Read:  “All Scripture is breathed out by God and profitable for teaching, for reproof, for correction, and for training in righteousness, that the man of God may be complete, equipped for every good work” (2 Timothy 3:16-17). Challenge:  Knowing Jesus means knowing what He says. The Bible has everything you need to know about life and godliness. Take some time during the day to read your Bible. The book of John is a good place to start. Start slow, read a few verses and think them over. Look for what God has to say to you, promises he makes, or things He says about himself. Step 2: Be aware of God’s Character Truth:  No matter what, God is good! Read:  “Oh, taste and see that the Lord is good! Blessed is the man who takes refuge in him!” (Psalm 34:8). Challenge:  If God is truly good and love, then take ti...

MAFUNDISHO YA MWALIM MWAKASEGE AKIFUNDISHA KWENYE SEMINA

MAFUNDISHO YA SEMINA YA MWALIMU MWAKASEGE 
   AKIFUNDISHA KUHUSU FUNGUO ZA MBINGUNI.

“Nami nakuambia ….. na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:18 – 19).

Maneno haya ya Yesu Kristo yanatuonyesha kuwa, nia yake ni kulijenga kanisa lililo na mamlaka kuliko shetani. Kanisa ni mwili wake (Waefeso 1:22 – 23). Wakristo waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo ni viungo vya mwili wa Kristo – ni viungo vya kanisa (1 Wakorintho 12:12, 13, 27). Kwa hiyo Yesu Kristo anaposema atalijenga kanisa lake wala milango ya kuzimu haitalishinda – ana maana ya kuwa, kila mkristo aliye wake anajengwa kiroho awe na mamlaka ya kumshinda shetani.kwenye kila majaribu  unayo pitia hata kama ni magumu kiasi gani.

Ni budi tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufungue kama hakuna kitu cha kukifungua. Hawezi kutuambia tufunge kama hakuna kitu cha kufunga. Kwa hiyo ni lazima kuna vitu vya kuvifunga na kuna vitu vya kuvifungua.

Pia, tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufunge na kufungua kabla hajatupa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo. Uwezo na mamlaka tunapata ndani ya Kristo aliyetukabidhi funguo za ufalme wa mbinguni.

Itakuwa haina maana kwa Yesu Kristo kutukabidhi funguo bila ya kutufundisha namna ya kuzitumia. Hawezi kutukabidhi mamlaka bila kutufundisha namna ya kuyatumia.

Yesu Kristo anasema tukifunga au tukifungua, mbinguni nako kunatia mhuri kitendo hicho. Hatuwezi kufanya hivyo kama tulichokifanya hakifanani na mapenzi yake. Ndiyo maana tunaomba kuwa mapenzi yake yatimizwe hapa duniani, kama yanavyotimizwa huko mbinguni. Kwa maneno mengine tunaweza kusema ya kuwa ukifanya kitu chochote katika mapenzi ya Mungu, Ufalme wa mbinguni utakuwa upande wako.

1.   
Aina za Funguo:

Biblia inazungumza juu ya funguo za aina tano zifuatazo: kama zifuatanzo na ukizisoma kwa makini na kuziweka kwenye matendo utauona mkono wa bwana ukikuonekania maishani kwako mote  na wala milango ya kuzimu haitakushinda

1. Funguo za Ufalme wa Mbinguni – Mathayo 16:19 – Yesu Kristo amekabidhi funguo hizi kwa wakristo (Kanisa).wote katika kanisa sasa usipo zitumia shetani atazitumia badala yako
2. Funguo za mauti na za kuzimu – Ufunuo 1:18 – Funguo hizi anazo Yesu Kristo – baadaye atampa Malaika mmoja funguo za kuzimu ili amfunge Ibilisi (Ufunuo 20:1-3).
3. Ufunguo wa nyumba ya Daudi – Isaya 22:22; Ufunuo 3:7. Ufunguo huu anao Yesu Kristo.
4. Ufunguo wa kawaida wa mlango – Waamuzi 3:25.
KUMBUKA BILA FUNGUO HAUTA WEZA KUFUNGUA BARAKA ZAKO AMBAZO ZIMEFUNGWA NA SHETANI

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUNENA KWA LUGHA HIZI HAPA

NAMNA YA KUFUNGA ILI UJIBIWE

ondoa jiwe iliujibiwe maombi yako