Piga shetani mpaka akuogope na akukimbie kwa juna la Yesu
- Get link
- X
- Other Apps
NILIVYOMTIMUA SHETANI "MKUKU-MKUKU", SIKU WALIYOZALIWA MAPACHA 202.
(STRATEGIES ZA KUMBANANISHA MUNGU PT.4)
Nadhani mnajua kwamba Mungu ametujalia (mimi na mke wangu), watoto mapacha wa kike na wa kiume. Mapacha 101 (Albertina na Alberta) na Mapacha 202. (Nathan na Nathanael), waliozaliwa, Mei mwaka huu.
Kuzaliwa kwa mapacha 202, hakukuwa rahisi maana Shetani alijihudhurisha kwa namna iliyonipa uzoefu mpya kabisa. Ukisikia zile habari za Yesu Kristo kupandishwa nyikani na Ibilisi ili ajaribiwe unaweza usielewe ama unaweza kudhani ni stori ya kudhahanika, may be mpaka siku utakapokutana na Ibilisi uso kwa uso.
Kama si Bwana aliekuwa upande wangu sasa hivi ningekuwa naongelea kuanua matanga ya msiba wa mke wangu. Wale tuliokesha pamoja tukipambana katika maombi siku ile, Eliah Geofrey Kamwela, brother Kotasi Mbwillo, (kuwataja wachache) ni mashahidi wa ushuhuda huu ninaokuletea leo.
NAOMBA UELEWE HILI KWANZA
Tangu nilipogundua kuwa kumshinda Shetani ni simpo sana kuliko hata kutafuta hela, Shetani na mikwara yake hajawahi kunisumbua kiwango kwamba nihofie kwa lolote.
Shetani mwenyewe ni shahidi jinsi ninavyomkimbizaga kila akijaribu kuleta fyokofyoko katika mambo yangu. Haiwezekani na haitakaa itokee, kwamba nimembeba Yesu Kristo ndani yangu halafu shetani anishinde kwa lolote. It cant hapen!
Shetani anachezaga na ufahamu ulionao katika Neno la Mungu, akigundua kwamba huna Neno la kutosha anajua atakubwaga. Shetani ni mwoga sana kwa watu waliojaa Neno la Mungu, maana anajua kwamba atafurukuta lakini mwisho wa siku atakimbizwa kirahisi.
SHETANI ALIVYONITOKEA!
Mke wangu alipokuwa labour (theatre),oparesheni ikiendelea, Shetani alikuja na kuniambia, "Albert hivi unajua kwamba kuzaa kwa oparesheni ni ishara kwamba nimekushinda kwa sababu, mtu unaemwamini Mungu mkeo inabidi ajifungue kawaida"
Nikamuuliza Shetani imeandikwa wapi? Akanijibu, "Wahubiri wengi wanasemaga" Nikamwambia, "Shetani acha ujinga, mimi siangalii mitazamo ya wahubiri bali ninaangalia Neno linavyosema". Akaniambia, imeandikwa wapi kuwa mwanamke atazaa kwa oparesheni?". Nikamwambia, "Katika ISAYA 66:7, imeonesha kwamba mwanamke anaweza kuzaa kabla ya utungu (oparesheni)". Shetani akanywea!
Alipoona nimemjibu hivyo, akaja tena na kuniambia, "Hivi unajua oparesheni ni hatari sana lwa sababu lolote laweza kutokea, ukapoteza mke ama watoto (maana walikuwa mapacha?". Nikamwambia, "Shetani acha kunisumbua, kwa sababu imeandikwa katika KUTOKA 23:26 ya kwamba hakutakuwa na vifo vya watoto na wala mke wangu hawezi kufa kwa sababu hajafika miaka 100 na Mungu ananiambia katika ISAYA 65:20 kwamba mke wangu akifa kabla ya miaka 100 ni laana. Mimi na mke wangu na watoto wetu hatupo chini ya laana kwa sababu Kristo alitukomboa dhidi ya kila laana, Wagalatia 3:13"
KIMBEMBE KIKATOKEA!
Nikiwa nimemaliza kumpa hoja hizo Shetani, mara nikapigiwa simu na daktari ya kwamba mke wangu amepungukiwa damu na kwamba isipopatikana uwezekano wa yeye kuishi ni mdogo. Hiyo ilikuwa majira ya saa saba usiku na nilikuwa hapo hospitali. Juhudi za kutafuta damu zikagonga mwamba kwa sababu group lake lilikosekana.
Ghafla Shetani akanirudia tena na akafanya timbwili sio haba. Akaanza kwa kusema, "Albert nilikueleza kwamba theatre si mahali salama, umeona sasa?". Nikashtuka. "Then akanionesha jeneza lenye mwili wa mke wangu likiingizwa nyumbani mwetu na watu kibao wakinipa pole, kwanza kwa kufiwa na mke na pili kwa kibarua kilichopo mbele yangu cha kulea watoto wanne wadogo".Hiyo ilikua inaelekea saa nane usiku.
Machozi yakiwa yananitoka nikamsikia Shetani ananiambia, "Albert, mshukuru Mungu kwa kila jambo", kabla hata sijamjibu nikaona ananieleza kingine cha ajabu, "Albert wala usiwaze, maana kubali kwamba Neema ameshakufa, kwani Mungu atakupatia binti mzuri na mwema kulilo Neema na atawalea watoto wako vizuri sana".
Nikiwa bado nashangaa, nikaona amenipitishia picha nne za mabinti ninaowafahamu na kuniambia, "Katika hawa utamuoa mmoja wapo. Sasa hivi endelea tu kuwaza jinsi utakavyoendesha msiba huu wa mkeo".
Ghafla nikapata hasira moja ya hatari, Roho Mtakatifu akanichaji upya, nikafuta machozi na kuinuka nilipokua nimekaa nikasema, "Shetani stooooooop, umekatisha mstari mwekundu siwezi kukuacha salama". Hapo nilikuwa nimeyakumbuka mahubiri ya Bishop Oyedepo aliyonifundisha, jinsi ya kuhamisha milima na kifo. Kama kuna siku nimewahi kumuamuru shetani kwa mamlaka basi ile ilikuwa namba moja!
HASIRA YANGU ILIPOWAKA
Nikamwambia Shetani, "Yesu Kristo aliepo ndani yangu amenipa ahadi ya uzima na afya tele kwangu na kwa watu wa nyumbani mwangu (Matendo 2:39). Tena Yesu Kristo ninaemwamini na ambae yuko ndani ya mke wangu anadamu nyingi sana kiasi kwamba hadi ilimwagika na pia badala ya kutumia maji kutoa jasho, Yesu alitoa jasho la damu(Luka 22:44). Haiwezekani Yesu awe ma damu nyingi namna hii halafu mke wangu afe kwa kukosa damu, haiwezekani na haiwezi kutokea".
Nilikuwa najibizana ma Shetani kwa hasira kubwa sana, kutoka saa nane usiku hadi saa 11 alfajiri niliposikia Roho mtakatifu ananiambia, "Shetani amesalimu amri, amekuacha na amekimbia". Mke wangu, alitoka theatre akiwa na uhai, licha ya hali yake kuwa mbaya sana, lakini hadi naandika ushuhuda huu ni mzima asilimia 100, anadunda na watoto wote, Nathan na Nathanael wanaendelea vizuri kabisa.
NADHANI UNAELEWA KWAMBA:-
Siandikagi jambo hasa ushuhuda unaonihusu kama sina pointi ninazotaka uzikamate. Naomba ukamate pointi tano kubwa zifuatazo:-
1). Katika kusali kuna mambo mawili unatakiwa uyafahamu. Mosi kuna ile kumuendea Mungu kwa hoja, ndio tunaita maombi (prayer) lakini kuna ile kuhamisha milima(changamoto, matatizo, ugumu ) na kumkimbiza Shetani, hiyo tunaita masafisho (confrotation) ama wengine wanaitaga maombi ya vita. Kwenye prayer unapanga hoja kwa hoja, lakini kwenye confrotation unakwenda kwa stailo ya piga nikupige. Ukichanganya madesa unaweza kubamizwa. Kuna mambo hutakiwi kumueleza Mungu, bali unatakiwa kutumia mamlaka na silaha yako (Neno) kumu-address Shetani. Usiende kwa Mungu ukaanza kusema, "Mungu nisaidie kumuondoa Shetani...", ni wewe unaetakiwa kumuamuru aondoke vinginevyo, atakumaliza mchana kweupe huku Mungu akikutazama.
2). Shetani ni muhuni sana, usipokuwa makini atatumia maandiko haya haya ya Biblia kukupumbaza usipambane nae. Kwangu alikuja akaniambia, "Nimshukuru Mungu kwa kila jambo, (1Thes 5:18)", lengo lake lilikuwa kunipumbaza nikubali picha ya kifo cha mke wangu ili aende mbele za Mungu na kumweleza kuwa kifo kitokee kwa sababu nimekiri na kukithibitisha. Uwe mwangalifu! (1Petro 5:8)
Utaenda hospitali watakupa ripoti kuwa una ugonjwa usiopona na kwamba uishi nao kwa matumaini na shetani atakwambia, "usiwaze maana wanaoumwa kama wewe wako wengi". Mwambie imeandikwa, "Kwa kupigwa kwake mimi nimepona". Usiingie kwenye mtego wa kukubaliana na matokeo eti kisa vipimo vimeonesha kwamba huwezi kuzaa, mwambie Shetani, imeandikwa katika (Kutoka 23:26) ya kwamba hutakuwa tasa, no matter what!
Habari ya kwamba siku hizi hali ni ngumu na kila mtu analalamika, mwachie Shetani mwenyewe kwa sababu wewe ni mtoto wa ahadi kama Isaka (Galatia 4:28) na Isaka alifanikiwa wakati wengine walipokuwa wanaisoma namba kule Ufilistini,(Mwanzo 26:12-14) kwa hiyo, asikubabaishe na usikubaliane nae akikuonesha picha ya kwamba unaisoma namba kwa maisha magumu. I beg you mno, usikubali Shetani akakuweka chini kwa namna yeyote katika hali yeyote. Simama kiume, pambana nae kwa Neno na atakukimbia tu (Yakobo 4:7)
3). Shetani huwa anafahamu shuhuda kubwa zilizopo mbele yako, hivyo huwa anajaribu kuziua mapema kabla haujashangilia. Unaweza kupiga picha, ikiwa ningekuwa na furaha yeyote kama mke wangu angekuwa amekufa na nimebakiwa na ushuhuda wa mapacha double double. Ni wazi kwamba ningetumia muda mwingi kumwombolezea mke wangu badala ya kushangilia muujiza wangu, na hapo shetani angekuwa amepiga bao. Huu mtindo shetani hajauanza leo, alishafanyaga hata kwa Yesu Kristo. Yesu alipoazaliwa alitambua kwamba angeleta madhara kwake, hivyo akaamua kumtumia Herode ili amuangamize.
Shetani anajua kwamba umesubiri mtoto kwa muda mrefu na kwamba umeshadharauliwa, umeshasemwa, umeshatemewa mate na kung'ongwa sana kisa huzai. Shetani anajua kwamba siku ukipata mtoto, itakuwa ni aibu kwake, kwa hiyo anakazana ili kwamba usipate mtoto.
Na akiona hawezi kuzuia usipate mtoto, atajaribu kuvuruga ndoa yako msielewane vizuri na mwenzi wako (kisa mtoto kachelewa), na mtoto atakapokuja, shetani anataka uje utumie muda mwingi kuumia kwa ajili ya ndoa ambayo haijakaa vizuri badala ya kushangilia muujiza wa kupata mtoto uliemngojea kwa muda mrefu. Si unaouona uhuni wake?
Pia shetani huenda amebana kiasi kwamba hadi sasa hivi umri wako ni miaka juu ya thelathini na bado hakuna dalili zozote za kuolewa kwako. Anajua hilo ndilo unalosubiri kwa hamu-yaani kuolewa. Akishaona hawezi kukuzuia usiolewe atatangulia mbele kukuzuia usipate mtoto. Badala ya uwe unashangilia muujiza wako (yaani kuolewa) utajikuta unaanza kuhuzunika kwa kukosa mtoto. Shetani anaitwa testimonies robber (yaani mwizi wa shuhuda). Usimchekee!
Kwa changamoto yeyote unayopitia, mwambie Shetani, nitatoka salama, kila kitu changu kikiwa salama na wala huwezi kuniabia lolote mahali popote. Ushuhuda wetu (mimi na mke wangu), wa kupata mapacha mfululizo tena wa kike na kiume, unawainua maelfu na ndio maana shetani alipambana nao kwa gharama zote ili usitokee. Mimi alinigwaya, kwa sababu nilitoka salama. Tazama! Mke wangu mzima, watoto wangu wazima. Aibu kwake shetani na utukufu kwa Mungu wetu, juu mbinguni.
4). Moja ya mambo yatakayokufanya umkimbize shetani kiurahisi ni uvumilivu. Hakikisha unakomaa mwanzo mwisho mpaka uone amesarenda. Mume wako ameingiwa na pepo la michepuko, unasali miezi miwili mitatu unaona habadilili eti unakata tamaa na kuanza kutafuta wa kukupooza nje ya ndoa. Haa! Umemuomba Mungu akupe mtoto/watoto kisa huu ni mwaka wa tatu tangu mmefunga ndoa, unaanza kushawishika kwenda kwa waganga wa kienyeji kisa unadhani Mungu kachelewa. Umeomba kazi huku na kule umekosa na suluhu umeona ni kutoa rushwa ama kuhonga ili uajiriwe. Kwa staili hiyo, shetani ataendelea kukuchezea.
Take it from me, ukiingia magotini kumsihi Mungu, ama ukiingia vitani kulambana na shetani kwa kuwa anakuzuia usipokee unachotakiwa kupokea, hakikisha hutoki magotini mpaka Mungu amejibu na hakikisha huweki silaha chini mpaka Shetani amesalimu amri na kuachia alichokibana.
5). Linapokuja suala la imani mbele za Mungu, nakusihi sana uwe "mtata" ama wakoloni wanasema uwe "aggressive". Shetani asikunyanyase kwa namna yeyote. Achana kabisa na yale maombi ya kikondoo ya kusema, "Mungu kama ni mapenzi yako naomba unijibu na kama sio mapenzi yako nitashukuru". Weeeeeee! Haujasoma katika maandiko ya kwamba mapenzi ya Mungu kwako kuhusu kila jambo yanajulikana? (Yeremia 29:11). Kabla hujamwendea Mungu ama kabla hujamgeukia shetani hakikisha kwamba unafahamu mapenzi ya Mungu kuhusu ishu inayokusumbua. Na hapa ndipo ulipo umuhimu wa kujaa Neno la Mungu mapema.
Kitu kitakachokuokoa siku ya kupambana na shetani ni maandiko na Neno, vilivyojaa ndani yako, na si vinginevyo! Shetani akipiga, unapiga! Akiweka, unaweka, mpaka anyooshe mikono. Nyie mnaoaminigi kwamba oparesheni wakati wa uzazi ni laana, iweni makini sana, maana kuna siku shetani anaweza kukitumia mnachoamini na akawapeleka mahali pema peponi! Alishajaribu kuniulia mke wangu kwa imani hii, kama sio Neno la Mungu na la maarifa kuhusu oparesheni lililokuwa ndani yangu, huenda ingekuwa habari nyingine sasa!
NI KWAMBA:-
Kama kuna ishu imekutesa muda mrefu na umekuwa ukipeleka hoja kwa Mungu na huoni majibu, hebu weka pozi kwanza. Ichunguze ishu yenyewe uone kama inabidi upeleke hoja kwa Mungu ama umfurumushe Shetani. Ninatambua kwamba mpo wengi ambao mmesubiri watoto kwa muda mrefu, mmesubiri mdoa zitengemae kwa muda mrefu, mmesubiri ajira muda mrefu, mmesubiri kuolewa muda mrefu, mmesubiri maisha yakae sawa muda mrefu na huenda mmekuwa mkimlilia Mungu pasipo majibu.
Leo hii, fanyeni uchunguzi, huenda imewapasa muelekeze mashambulizi kwa shetani moja kwa moja. Ikiwa ni ishu ya kumwandamisha shetani, ninawahakikishia kwamba mkitumia mbinu nilizotumia kuhakikisha uhai wa mke wangu unahifadhiwa, hakika mtaniletea ushuhuda wa kuinuliwa kwenu muda si mrefu kuanzia sasa
Comments